13.Faida Katika Hadeeth ya Jibriyl-08


(6). Ni kwamba shetani katika kuwapotosha watu ana njia kuu mbili:
(1). Yule ambaye anayapuuzia mambo ya twa’ah na kuwa na mapungufu, huyu anampambia mambo machafu (shahawāt).
Na alisema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam):

“حفت الجنة بالمكاره وحفت النار بالشهوات”

رواه البخاري (٦٤٨٧)، ومسلم (٢٨٢٢)

“Imezungushiwa pepo mambo yanayochukiza, na umezungushiwa moto mambo machafu (shahawāt).
Ameipokea Bukhari (6487) na Muslim (2822).
Na mwenye hili huambiwa ana maradhi ya Shah-wah (matamanio).
Na katika hilo imekuja kauli yake Allāh Mtukufu:

فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ     ” الأحزاب ٣٢

“Basi msilegeze sauti kwani watatumai wale ambao kwenye mioyo yao kuna maradhi” Ahzāb (32).
(2). Ama yule ambaye atakuwa ni miongoni mwa watu wa twa’ah na ibadah, huyu atajiliwa na shetani kupitia njia ya kupituka mipaka katika hiyo ibadah na kumtupia mambo tata (shubhah).
Amesema Allāh-‘Azza Wajalla-:

هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ ۖ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ     ” آل عمران٦

“Yeye (Allāh)/ndiye ambaye amekuteremshia wewe kitabu ndani yake kuna ayah zilizo wazi ambazo ni msingi wa (hicho) Kitabu. Na nyengine zatatanisha. Ama wale ambao kwenye mioyo yao kuna kumili kuiacha haki wao hufata zile zinazotatanisha kwa lengo la kutaka kupoteza (watu), na kwa lengo la kutaka kuzipondoa (maana iliyokusudiwa)”. Al-‘Imrān (06).
Na imekuja hadithi katika sahihi ya Imam Bukhari (4547), na Muslim (2665), kutoka kwa mama ‘Aisha (Allāh amridhie), kwamba Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) aliisoma (siku moja) ayah hii, kisha akasema:
“Pindi mtakapowaona wale ambao wanafata zile zenyekutatanisha (katika ayah) basi hao ndio wale aliowataja Allāh kaeni nao chonjo”.
Na humabiwa mwenye hili ana maradhi ya shubhah.
Na katika hilo imekuja kauli yake Allāh Mtukufu:

فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّهُ مَرَضًا ۖ      ” البقرة ١٠

“Kwenye mioyo yao kuna maradhi na Allāh akawazidishia maradhi” Al-Baqarah (10).
Na kauli yake Allāh Mtukufu:

“وَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَتْهُمْ رِجْسًا إِلَىٰ رِجْسِهِمْ    ” التوبة ١٢٥

“Ama wale ambao kwenye mioyo yao kuna maradhi basi zitawazidishia (hizi ayah) uchafu juu ya uchafu waliokuwa nao” Al-Tawbah (125).
Na watu wa aina hii ndio wale aliuoulizwa Ibn ‘Umar. Na Yahya bin Ya’mar alipotaja wasifu wao alisema ni watu wa ibadah, akasema:
“Wamedhihiri pande za kwetu watu wanasoma (sana) Qur’an, na wamebobea katika elimu”.
na akataja na sifa zao nyengine.
Na hawa na mfano wao katika watu wa bida’ah hujiliwa na shetani kwa lengo la kuwapoteza kupitia njia ya shubhah.
 
 
Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim:http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: sharh Hadithi Jibriil