16.Faida Katika Hadeeth ya Jibriyl-11


(9). Kauli yake aliposema (Allāh amridhie):
“Siku moja tulipokuwa tumekaa mbele ya Mtume wa Allāh (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam), ghafla akatutokea bwana mmoja aliyevaa nguo nyeupe mno mwenye nywele nyesi mno ambaye haionekani juu yake athari ya safari na wala hakuna yeyote miongoni mwetu amjuaye. Akaishilia kuketi mbele ya Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam), na akayakutanisha magoti yake sanjari na magoti ya Mtume wa Allāh (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam), na akaweka mikono yake juu ya mapaja yake…”
Kisha akamuuliza kuhusu Uislam, Iymān, Ihsān, kiyama na alama zake. Na akasema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) baada ya hayo:
“Hakika yule ni Jibriil amekujieni ili awafunze Dini yenu “.
Zipo faida nyingi ndani yake.

Ya kwanza:

Imekuja hadithi katika sahihi Bukhari (50) na Muslim (9) kutoka kwa Abū Hurayrah (Allāh amridhie) amesema:

“كان النبي صلى الله عليه وسلم بارزا يوما للناس”

“Alikuwa Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) siku moja amebarizi mbele za watu”.
Na katika sunan Abiy Daud (4698) kwa Isnadi sahihi kutoka kwa Abū Dharr na Abū Hurayrah wamesema:

كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يجلس بين ظهراني أصحابه، فيجيئ الغريب فلا يدري أيهم هو حتى يسأل، فطلبنا إلى رسول الله صلى الله عليه وسلم أن نجعل له مجلسا يعرفه الغريب إذا أتاه، قال: فبنينا له دكانا من طين، فجلس عليه، وكنا نجلس بجنبتيه

“Alikuwa Mtume wa Allāh (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) anakaa katikati ya Maswahaba wake, kisha anapokuja mtu mgeni hajui kati yao Mtume ni nani mpaka amuulizie. Tukamuomba ruhusa Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) tumtengezee majlis ambayo akikaa atajulikana pia na mtu mgeni atakapomjia. Tukamtengenezea kibaraza cha udongo akawa anakaa juu yake, na sisi tukawa tunakaa pembeni mwake”.
Na katika hili kuna dalili juu ya kwamba inatakikana kwa mwalimu awe katika sehemu yenye muinuko ili ajulikane na wamuone wote, hasa hasa pale mkusanyiko utakapokuwa mkubwa, ili waweze wote kustafidi kutoka kwake.
 
 
Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah