17.Faida Katika Hadeeth ya Jibriyl-12


Ya pili:

Ni kwamba Malaika huwajia wanaadamu kwa umbile la ki-binaadam.
Na mfano wa hilo ni yale yaliyokuja katika Qur’an ujio wa Jibriil kwa mama Maryam katika umbile la mwanaadam.
Na ujio wa Malaika kwa Ibrahim na Luut katika umbile la ki-binaadam.
Na wao wanajigeuza hivyo kwa uwezo wa Allāh-‘Azza Wajalla- wanajibadili kutokana na umbile waliloumbiwa kwenda kwenye umbo la ki-binaadam.
Na hakika Amesema Allāh-‘Azza Wajalla- katika umbile la Malaika:

الْحَمْدُ لِلَّهِ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ جَاعِلِ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا أُولِي أَجْنِحَةٍ مَّثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۚ يَزِيدُ فِي الْخَلْقِ مَا يَشَاءُ ۚ     ” فاطر ١

“Sifa zote njema anastahiki Allāh Muumba wa mbingu na ardhi, aliyewajaalia Malaika kuwa na Mitume,(wao) wana mbawa mbili mbili tatu tatu na nne nne, anamzidishia umbile (la mbawa) amtakaye” Fātir (1).
Na imekuja katika sahihi ya Bukhari (4857), na Muslim (280), kwamba Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) alimuona Jibriil akiwa na mbawa mia sita.
Na mfano wa Malaika katika kule kuja kwao kwa umbile la binaadamu ni majini.(yaani majin pia huja katika umbile la binadam) Kama ilivyothibiti katika sahihi Bukhari (2311) kutoka kwa Abū Hurayrah (Allāh amridhie), katika kisa cha yule aliyekuwa anamjia na kuiba chakula.
Na kama wanavyokuja katika umbile la ki-binaadamu pia huja kwa umbo la Nyoka. Kama ilivyokuja hadithi katika sahihi Muslim (2236).
Na Malaika na Majini kwa umbile lao wanawaona watu kwa namna ambayo (watu) hawawezi kuwaona.
Na hakika amesema Allāh-‘Azza Wajalla-, kuhusu Majini:

 “إِنَّهُ يَرَاكُمْ هُوَ وَقَبِيلُهُ مِنْ حَيْثُ لَا تَرَوْنَهُمْ ۗ      ” الأعراف٢٧

“Hakika yeye anakuoneni, yeye na kizazi chake, kwa namna ambayo nyinyi hamuwezi kuwaona wao” Al-A’rāf (27).
 
 
Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim:http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Sharh Hadithi Jibriil