44.Msingi wa al-walaa wal-baraa-01


(1).  Kama atakuwa mja amehakiki (na kupatikana kwake) shuruti za لا إله إلا الله , na akampenda Allāh  na Mtume wake, mpaka akawa Allāh  na Mtume wake wanapendeza zaidi kwake yeye kuliko mwengine yeyote mpaka nafsi yake.  Na akawapendelea Waumini kile akipendacho nafsini mwake, na akajitakasa na kujiweka mbali kutokana na ukafiri na watu wake, na akawafanya kuwa ni maadui kwaajili ya Allāh uadui uliotimu kwa sababu ya ukafiri wao.  Huyo ni muumini mkamilifu wa Iymān, aliyetenda ya wajibu na akayaacha ya haramu.
(2).  Na kama mja ataipatikanisha Iymān ya wajibu, kisha akafanya ya ziada kwa kufanya mambo ya Sunnah na kujiepusha na yanayochukiza (makruuhāt), huyu atakuwa ni mkamilifu zaidi  kwakuyazidisha yale  ya Sunnah.
Na amesema Allāh  Mtukufu katika hadithi Qudsiyy:

“وما تقرب إلي عبدي بشيئ أحب إلي مما افترضته عليه، وما يزال عبدي يتقرب إلي بالنوافل حتى أحبه”

رواه البخاري

“Na wala hatojikurubisha kwangu mja wangu kwa jambo ambalo lapendeza zaidi kwangu kuliko (mja wangu kulifanya) nililolifaradhisha (nilolilazimisha)  juu yake.  Na hatoachakuwa mja wangu anajikurubisha kwangu kwa yale ya sunnah (ambayo sijamlazimisha) mpaka nimpende”.
Ameipokea Bukhari.

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah