51.Kuwapenda Waumini na Kuwanusuru na Tahadhari Juu ya Kukhalifu Hilo-04


(d). Usimdharau ndugu yako Muislam, wala usimtelekeze, wala usimsalimishe kwa maadui.
Na hakika amesema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam):

المسلم أخو المسلم لا يظلمه ولا يخذله ولا يحقره التقوى هاهنا ويشير إلى صدره ثلاث مرات بحسب امرئ من الشر أن يحقر أخاه المسلم كل المسلم على المسلم حرام دمه وماله وعرضه

رواه مسلم عن أبي هريرة رضي الله عنه

“Muislam nduguye ni Muislam (mwenzake), hamdhulumu, hamtelekezi wala hamdharau. Uchamungu upo hapa- Akawa anaashiria kifuani mwake mara tau- imetosha kwa mtu kuhesabika kuwa ni mja wa shari pale anapomdharau ndugu yake Muislam. Kila Muislam kwa Muislam ni haramu damu yake (kuimwaga) na mali yake (kuichukua bila ya ridhaa) na heshima yake (kuivunja)”.
Ameipokea Muslim kutoka kwa Abū Hurayrah (Allāh amridhie).

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah