58.Kuwapenda Waumini na Kuwanusuru na Tahadhari Juu ya Kukhalifu Hilo-11


(k). Zuilia uharibifu na khasara ya ndugu yako na umuhifadhi nyuma yake.
Kama alivyosema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) katika hadithi ya Abū Hurayrah (Allāh amridhie):

“المؤمن مرآة المؤمن، والمؤمن أخو المؤمن، يكف عليه ضيعته، ويحوطه من ورائه”

رواه أبو داود (حسن)

“Muumini ni kioo cha Muumini, na Muumini ni ndugu wa Muumini, anamzuilia khasara zake na anamlinda nyuma yake”.
Ameipokea Abū Daud (hasan).

 

قال مقيده-عفا الله عنه

MAELEZO:

Wanasema ‘Ulamaa (Allāh awarham):
Muumini kuwa ni Kioo cha Muumini mwenzake ni kule kuwa mtu atazijua shida na aibu za nafsi yake kwa kujuzwa na kunasihiwa na ndugu yake, kama vile anavyoona dosari zilizopo usoni mwake kwakujitazama kwenye Kioo.
Na huu ndio wajhi na maana ya maneno ya Amiiril-Mu’miniin ‘Umar bin Al-Khattwāb (Allāh amridhie) alipokuwa akisema:

رحم الله امرأ أهدى إلي بعيوب نفسي

“Allāh amrahamu mtu ambaye atanizawadia (kwa siri) aibu za nafsi yangu”.
Na kumzuilia Muumini mwenzio khasara, ni kwenye mali yake ukiona itakumbwa na khasara au kuharibika na wewe upo basi jitahidi ufanye jambo isiharibike mali ya ndugu yako, pia huingia hapo kumlindia kazi yake ambayo unaona kuwa wapo watu wanadhamira naye mbaya.
Na kumlinda nyuma yake, kwa maana anapokuwa ameondoka (mathalan) usikubalia atetwe na asengenywe mbele yako, pia usikubali apangiwe njama mbaya mbele yako.

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah