60.Kuwapenda Waumini na Kuwanusuru na Tahadhari Juu ya Kukhalifu Hilo-13


(m). Na wakuamini watu, miongo mwao ni Waumini, juu ya damu zao, mali zao na nafsi.
Na hakika amesema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) katika hadithi ya Fadhālah bin ‘Ubayd (Allāh amridhie):

“المؤمن من أمنه الناس على أموالهم وأنفسهم والمهاجر من هجر الخطايا والذنوب”

رواه ابن ماجة

“Muumini (wa kweli) ni yule atakayeaminika na watu juu ya mali zao na nafsi zao. Na aliyefanya hijrah (aliyehama) ni yule aliyeyahama makosa na madhambi”.
Ameipokea Ibn Mājah (sahihi).

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah