62.Kuwapenda Waumini na Kuwanusuru na Tahadhari Juu ya Kukhalifu Hilo-15


(o). Kuwa ni kitu kimoja na Waumini dhidi ya wasiokuwa Waumini.
Na hakika amesema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) katika hadithi ya ‘Aliyy (Allāh amridhie):

“المؤمنون تتكافأ دماؤهم ويسعى بذمتهم أدناهم وهم يد على من سواهم”

رواه أبو داود والنسائي

“Waumini (wote) zinakuwa sawa damu zao, na anasimamia wachini wao dhima zao, na wao ni mkono mmoja kwa wasiokuwa wao”.
Ameipokea Abū Daud na Al-Nasāiy (sahihi).
Na imekuja katika hadithi ya ‘Abdillāh bin ‘Amri (Allāh awaridhie):

“المسلمون تتكافأ دماؤهم…” وفيه: ” يرد مشدهم على مضعفهم ومتسريهم على قاعدهم..”

رواه أبو داود وابن ماجة

“Waislam wote huwa sawa damu zao”.
Na ikaja pia:
“Atarudisha mshupavu wao juu ya mnyonge wao, na waliotoka kwa waliobakia”.
Ameipokea Abū Daud na Ibn Mājah (hasan).

 

قال مقيده -عفا الله عنه

Wanasema ‘Ulamaa (Allāh awarham):
Maana ya kuwa sawa damu za Waumini na Waislam ni katika diya na kisasi.
Atalipiziwa kisasi mtu mwenye hadhi kwa mtu mnyonge, mkubwa kwa mdogo, mjuzi kwa mjinga, mwanamke kwa mwanamme.
Kwa maana: mwenye hadhi atakapomuua mnyonge basi naye atauawa, kwa sababu damu zao zipo sawa.
Na kusimamia wachini wao dhima zao ni pale mtu aliyeduni katika Waislam atakapompa amani na kumpokea mgeni asiyekuwa Muislam (mathalan) katika mji wa Waislam, basi hana fursa yeyote kutengua wala kupinga hilo.
Na kurudisha mshupavu wao kwa mnyonge wao, ni Mujāhid katika Mujaahidiina mwenye mabavu na nguvu akipata ngawira basi itamuhusu ngawira hiyo hata yule ambaye ni mdhaifu katika mapigano kwakuwa wote wanafanana na dhima yao ni moja.
Na waliotoka kwenye Jihadi watashirikiana kwenye ngawira na wale waliobakia katika ulinzi wa mji na ngome yao.

والله أعلم

 
 
Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah