64.Kuwapenda Waumini na Kuwanusuru na Tahadhari Juu ya Kukhalifu Hilo-17


(q). Bainisha aibu (dosari) katika bidhaa unayomuuzia ndugu yako Muislam.
Na hakika amesema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) katika hadithi ya ‘Uqbah bin ‘Aamir (Allāh amridhie):

“المسلم أخو المسلم لا يحل لمسلم باع من أخيه بيعا فيه عيب إلا بينه له”

رواه أحمد وابن ماجة والترمذي

“Muislam ni ndugu wa Muislam, haiwi halali kwa Muislam atakayemuuzia nduguye bidhaa yenye aibu ila anatakiwa ambainishie”.
Ameipokea Ahmad na Ibn Mājah (sahihi).
 
 
Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah