01.Utangulizi


بسم الله الرحمن الرحيم

الحمد لله رب العالمين، والصلاة والسلام على المبعوث رحمة للعالمين، نبينا وسيدنا وقدوتنا محمد، وعلى آله الطيبين الطاهرين، وعلى أصحابه الغر الميامين، ومن تبعه بإحسان واقتفى سنته إلى يوم الدين

أما بعد

Hii ni risala tunayoitanguliza kwa kila mwenye akili aliye mwerevu, anayeitanguliza akili yake juu ya matamanio, na kuipa haki kipaumbele kuliko maasi, anayeijua haki kupitia haki na wala haijui haki kupitia watu, anayejua kuwa haki ina haki zaidi kufatwa.
Na tumeipa jina liitwalo:

رسالة إلى محبي آل البيت

“Ujumbe kwa wapenzi wa Ahlul-Bayt”.
Na risala hii imechukuliwa kutoka katika vyanzo tegemewa vya shia.
Kwa sababu shia ni sawa na mapote mengine, wapo miongoni mwao wenye akili wanaopenda kheri na kuishikilia, na kama ataoneshwa basi ataikubali kwa idhini ya Allāh.
Na wapo miongoni mwao ambao wametanguliza ung’ang’anizi na uigaji (wa kimakosa) dhidi ya haki. Hivyo wakaziharibu akili zao (zikashindwa kufikiri) na wakafata matamanio ya nafsi zao, na wakawaiga wenziwao pasi na hoja wala elimu yoyote kutoka kwa Allāh.
Na hakika sisi tunatamani kutoka kwa msomaji wa ujumbe huu aupokee kwa kifua kipana na akili iliyofunguka na kuipa haki nafasi yake, kwani haki ni kitu cha thamani mno popote itakapokuwa na kutoka kwa yeyote.

 

 

Muhusika: El-Bāhithiin fil-Muntaqaa
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Ilaa Muhibbiy Aalil-Bayt Uk.3-4