06.Ujumbe kwa Wapenzi wa Ahlul-Bayt-05


Ahlul-Bayt kujiita kwa jina la ‘Aisha:
Miongoni mwa walioitwa ‘Aisha katika ukoo wa Aliyy (Allāh amridhie):
▪’Aisha bint Imam Ja’far Al-Swādiq.
▪’Aisha bint Muwsā Al-Kādhim.
▪’Aisha bint Ja’far bin Muwsā Al-Kādhim.
▪’Aisha bint Aliyy Al-Ridhaa
▪’Aisha bint Aliyy Al-Hādiy.
▪’Aisha bint Muhammad bin Al-Hasan bin Ja’far bin Al-Hasan Al-Muthanna.
Hivi hawakuwa Ahlul-Bayt kwa shia ni kiigizo chema katika kila jambo?
Hivi wafuasi wao wataweza kuwaiga katika kuwaita kwa majina haya vijana wao na binti zao?
Ni kweli ataweza kupata ujasiri shia juu ya kumwita mtoto wake kwa jina la Abūbakr? ‘Umar? ‘Uthmān? Au kumwita binti yake kwa jina la ‘Aisha? [1].

 

—————————
[1] Jawabu ni kuwa hawawezi, na tumeshuhudia hilo kwa mashia wengi hapa Tanzania kubadilisha majina yao, miongoni mwa hao ni Omar Jumaa Mayunga aliyedhihirisha wazi kuwa jina la Omar ni la kikafiri, hivyo akalikana jina alilopewa na wazazi wake na kujibatiza jina la ‘Aliyy Jumaa Mayunga, na hili ameliandika kwenye tafsiri yake ya kiswahili.
 
 
Muhusika: El-Bāhithiin Fil-Muntaqaa
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Ilaa Muhibbiy Aalil-Bayt Uk. 6-7