10.Ujumbe kwa Wapenzi wa Ahlul-Bayt-09


3- Hutaja vyanzo vya shia kuwa Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam), aliwapasha khabari watu wa nyumbani kwake (Ahlul-Bayt), kwa maudhi watakayoyapata kutoka kwa watu, kwa sababu Allāh Mtukufu alishamjuza yote yatakayotokea baada yake mpaka siku ya kiyama. Lakini shia katika vitabu vyao tegemewa wanajenga hoja juu ya kuritadi kwa Maswahaba kupitia hadithi ya hawdhi isemayo:

“إنك لا تدري ما أحدثوا بعدك، إنهم لم يزالوا مرتدين على أعقابهم     “[١]

“Hakika wewe hujui waliyozusha baada yako. Hakika wao hawakuachakuwa ni wenye kuritadi na kurudi nyuma kwa visigino vyao” [1].
Hivi haya kuwa haya maneno ni dalili juu ya kwamba Mtume wa Allāh (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) hayajui yanayojiri baada yake!?
Na ikiwa Mtume wa Allāh (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam), hajui ghaibu basi asiyekuwa yeye ni zaidi kutokuijua ghaibu.

 

——————–
[1] متفق عليه عند أهل السنة. ورواه المجلسي في البحار ٨ ص ٢٧ و ج ٢٣ ص ١٦٥ وج ٢٨ ص ٢٧ وغيرها

 

 

Muhusika: El-Bāhithiin Fil-Muntaqaa
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Ilaa Muhibbiy Aalil-Bayt Uk.10