14.Ujumbe kwa Wapenzi wa Ahlul-Bayt-13


(7)- Kama kuna nguzo kuu za kimatendo katika Uislam basi ni swala.
Sasa iliwezekanaje kwa Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam), Abūbakr (Allāh amridhie), kusimama katika nafasi yake katika swala kipindi cha maradhi yake!?
Ilhali ‘Aliyy alikuwepo!?
Kwanini Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) amemtanguliza Abūbakr kuswalisha wala hakumtamguliza ‘Aliyy ilhali ndiye waswiyy wake na Khalifa wake kama wanavyoitakidi shia?
Na ikitokea kuwa Abūbakr alijitanguliza mwenyewe bila ya ridhaa Kwanini (Mtume swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) asimzuilie na kumuamrisha arudi nyuma kisha yeye ndo aswalishe? Kisha ajenge hoja kuwa (‘Aliyy) ndiye Khalifa atakayemkaimu Mtume wa Allāh baada yake na ni waswiyy wake (wala si Abūbakr)!!
 
 
Muhusika: El-Bāhithiin Fil-Muntaqaa
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Ilaa Muhibbiy Aalil-Bayt Uk. 11-12