24.Faida Katika Hadithi ya Jibriil-19


Yapili (alif):

Jambo la kwanza kabisa lililofasiriwa Uislām ni Shahada mbili, shahada ya kukiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kuwa hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allāh, na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allāh. Na shahada mbili hizi ni za lazima kwa kila mtu na jini kuanzia alipotumwa Mtume (swalla Llāhu’alayhi wasallam) mpaka kitakaposimama kiyama. Hivyo yeyote asiyemwamini Mtume (swalla Llāhu’alayhi wasallam) atakuwa ni mtu wa motoni, kwa ushahidi wa maneno yake (Swalla Llāhu’alayhi wasallam):
“Naapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad ipo mikononi mwake, hatonisikia yeyote katika Umma huu, awe myahudi au mkristo, kisha afariki wakati hajayaamini niliyotumwa nayo, ila atakuwa katika watu wa motoni”.
Ameipokea Muslim (240).

 

Muhusika: Shaykh’Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo Sharh Hadith Jibriil