17.Ujumbe Kwa Wapenzi Wa Ahlul-Bayt-16


10- Vitabu tegemewa vya shia vinakubaliana kuwa mahusiano baina ya ‘Umar na ‘Aliyy (Allāh awaridhie), yalikuwa ni ya chuki na kubugudhiana. Kisha tunakuja kuona kuwa huyu huyu ‘Umar anamtawalisha ‘Aliyy uongozi wa unaibu wake katika vita vyake vya Baytul-Maqdis. Na lau angeliuawa ‘Umar bila shaka angaendelea ‘Aliyy kuwa ni Khalifa aliyemkaimu (‘Umar).

 

Je, tendo hili alilolifanya ‘Umar linajulisha chochote katika kumchukia na kumbugudhi ‘Aliyy?

 

Na je, tendo la ‘Aliyy kukubali unaibu wa ‘Umar linajulisha juu ya kuwa ‘Umar alikuwa dhalimu muovu?

 

Hivi haiingii katika ufahamu (wa mwenye akili) kuwa kila mmoja miongoni mwa hawa alikuwa na mapenzi kwa mwenzake? Mwenye kumnasihi mwenzake? Na kwamba ‘Aliyy (Allāh amridhie) alikuwa miongoni mwa wanasihiji wa ‘Umar (Allāh amridhie)? Bali alikuwa ni katika mawaziri wake wakweli? Na kwamba ‘Umar mbele ya ‘Aliyy alikuwa ni kiongozi maridhawa aliyejuu ya uongofu?

 

 

 

 

 

Muhusika: El-Bāhithiin Fil-Muntaqaa

Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/

Marejeo: Ilaa Muhibbiy Aalil-Bayt Uk.13