30.Faida Katika Hadithi Ya Jibriil – 25


Yapili (خ):

Nia njema pekee haitoshi katika kuswihi kwa Ibada.
Na katika Sunan ya Imam Al-Dārimiy (1/68-69): Imekuja kuwa Abdullāh bin Mas-‘uud (Allāh amridhi):
“Aliwasimamia watu ambao walikaa msikitini wakiwa katika vikundi, mikononi mwao wana vichangarawe, mmoja wao anawaamuru na kuwaambia: Leteni Takbira mara mia moja, kisha wanaleta hizo takbira kwa idadi hiyo.
kisha anawaambia tena: Leteni Tahlili mara mia, moja, wao huleta tahlili mara hizo.
Kisha anawaambia: Leteni Tasbiih mara mia moja, wanaleta tasbiih mara hizo.
Akasema Ibn Mas-‘uud (Allāh amridhie): Ni yapi haya niyaonayo mkiyafanya?
Wakajibu: Ewe baba wa Abdirrahmaan! Hivi ni vichangarawe tunahesabu kwavyo Takbiir, Tahliil na Tasbiiih.
Akasema: Hebu hesabuni maovu yenu, mimi ntadhamini kutopotea kwa mema yenu chochote. Hivi mna nini nyinyi Umma wa Muhammad!? Kipi kimekupelekeeni muangamie haraka!? Hawa hapa Maswahaba wa Mtume wenu (swalla Llāhu’alayhi wasallam) wamejaa, na hizi hapa nguo zake hazijachakaa, na vyombo vyake havija vunjika. Na apa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake! Hakika mtukuwa nyinyi katika mila ambayo ni ongofu zaidi kuliko mila ya Muhammad (swalla Llāhu’alayhi wasallam), au mmekuja kufungua mlango wa upotevu.
Wakasema: Tunaapa kwa Allāh ewe baba wa Abdirrahmaan! Hatujakusudia (kwa haya tuyafanyayo) zaidi ya kheri tu.
Akasema: Na ni wangapi wanaoitaka kheri lakini hawaipatii!??”.
Na hii athar ameitaja pia Sheikh Al-Albāniy katika “Al-Sahiihah” (2005).
 
 
Muhusika: Shaykh’Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Sharh Hadith Jibriil