31.Faida Katika Hadithi Ya Jibriil – 26


Yatatu (alif):

Yenye umuhimu mkubwa katika nguzo za Uislām baada ya shahada mbili ni swala. Na aliisifia Mtume (swalla Llāhu’alayhi wasallam) kuwa ni Nguzo kuu ya Uislām, kama ilivyokuja katika hadithi ya wosia wake Mtume (swalla Llāhu’alayhi wasallam) kwa Mu’aadh bin Jabal, ambayo ni hadithi ya ishirini na tisa katika Arbaiin Nawawiyyah.
Na amehabarisha Mtume (swalla Llāhu’alayhi wasallam) kwamba swala ndiyo ya mwisho kabisa kupotea katika mambo ya Dini, na ni jambo la kwanza atakalohesabiwa mja juu yake siku ya kiyama.
Tazama “Al-Swahiiha” (1739), na (1358), na (1748) ya Sheikh Al-Albāniy.
Na kwamba kupitia swala hupatikana kipambanuzi baina ya Muislam na kafiri.
Ameipokea Muslim (134).
 
 
Muhusika: Shaykh’Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo:Sharhu Hadith Jibriil