33.Faida Katika Hadithi Ya Jibriil – 28


Yatatu (ت):

Katika ya mwisho aliyoyausia Mtume (swalla Llāhu’alayhi wasallam) ni swala.
Imepokelewa kutoka kwa Ummu Salamah (Allāh amridhie), kwamba hakika Mtume (swalla Llāhu’alayhi wasallam) alikuwa akisema kipindi cha maradhi yake yaliyosababisha kifo chake:
“Swalaa! Na vile mlivyomilikishwa kwa mikono yenu ya kuumeni”.[1]
Hakuacha kuyasema hayo maneno mpaka ulimi ukawa hauwezi tena kutamka na kubaini.
Na imepokelewa kutoka kwa Anas bin Mālik (Allāh amridhie) amesema:
“Ulikuwa wosia wa Mtume (swalla Llāhu’alayhi wasallam) pale alipohudhuriwa na hali ya umauti: “Swalaa! Na vile mlivyomilikishwa kwa mikono yenu ya kuumeni”.
Na kutoka kwa Aliyy bin Abiy Twalib (Allāh amridhie) amesema:
“Yalikuwa maneno ya mwisho ya Mtume (swalla Llāhu’alayhi wasallam): “Swalaa! Na vile mlivyomilikishwa kwa mikono yenu ya kuumeni”.
Na hadithi zote hizi ni sahihi amezipokea Ibn Mājah na wengineo, (1625), (2697), (2698).
———————
[1] Ambao ni Watumwa, ameusia watu waishi nao vyema, wasiwatese wala kuwanyanyapaa nk.
 
 
 
Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Sharh Hadith Jibriil