36.Faida Katika Hadithi Ya Jibriil – 31


Yatatu (ح):

Na hizi swala tano kuziswali kwake ni wajibu wa lazima kwa kila Muislam aliyebaleghe mwenye akili katika wanaume na wanawake, muda wakuwa roho (zao) zipo katika miili.
Na ni wajibu kwa wanaume kuziswali kwa jamaa Misikitini.
Na dalili juu ya hilo ni kauli yake Mtume (swalla Llāhu’alayhi wasallam) aliposema:
“Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake! Hakika nimepania kuamrisha moto ukokwe, kisha niamrishe swala ikimiwe, kisha nimuamuru mtu awaswalishe watu, kisha niwaendee watu kuwachomea nyumba zao. Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake! Lau angelijua mmoja wao kuwa atapata (akija Msikitini) mfupa wenye nyama iliyonona, au mishale miwili (midogo) iliyomizuri, bila shaka angelihudhuria swala ya ‘Ishaa”.
Ameipokea Bukhari (644), na Muslim (651), kutoka kwa Abū Hurayrah (Allāh amridhie).
 
 
Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Sharh Hadith Jibriil