39.Faida Katika Hadithi Ya Jibriil – 34


Yatatu (ذ):

Na amepokea pia katika Sahihi yake (653), kutoka kwa Abū Hurayrah (Allāh amridhie), kuwa amesema:
“Kipofu mmoja alimjia Mtume (swalla Llāhu’alayhi wasallam)[1] akasema: Ewe Mtume wa Allāh! Hakika sina mimi wakuniongoza kuelekea Msikitini. Akawa anamuomba amruhusu ili aweze kuswali nyumbani kwake, kisha akamruhusu. Alipogeuka kwa kutaka kuondoka Mtume (swalla Llāhu’alayhi wasallam) alimwita akamuuliza: Je, unaisikia adhana kwaajili ya swala? Akasema Ndiyo. Mtume (swalla Llāhu’alayhi wasallam) akamwambia: Basi uitike (wito wake, kwa maana njoo Msikitini)”.
———————
[1] Kipofu huyu ni Ibn Ummi Maktuum kama ilivyokuja katika “Sunan” ya Abiy Daud.
 
 
Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Sharh Hadith Jibriil