42.Faida Katika Hadithi Ya Jibriil – 37


Yanne:

Zaka ni mwenza wa swala katika Kitabu cha Allāh na Sunnah za Mtume wake (swalla Llāhu’alayhi wasallam), kama alivyosema Allāh ‘Azza wajalla-:

فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ    ” التوبة (٥)

“Kama watatubu na kusimamisha Swala na kutoa Zaka basi waachilieni njia zao”.
Al-Tawbah (5).
Na amesema:

فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ ۗ    ” التوبة (١١)

“Kama watatubu na kusimamisha Swala na kutoa Zaka basi hao ni ndugu zenu katika Dini”
Al-Tawbah (11).
Na amesema:

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ (٥)

“Na wala hawakuamrishwa ila kumuabudu Allāh hali ya kumtakasia yeye Dini, wanyenyekevu wakuepuka batili na kushikamana na haki, na wasimamishe Swala na watoe Zaka, na hiyo ndiyo Dini ya sawa sawa na Mila iliyonyooka”.[1]
Al-Bayyinah (5).
Nayo ni Ibada ya kutoa mali manufaa yake yanawafika wengine. Na amewajibisha Allāh kutoka katika mali za matajiir ambacho ni kiasi fulani cha kumnufaisha fakiri na wala hakimdhuru tajiri, kwa sababu ni kiasi kichache kwenye mali yake nyingi.
———————-
[1] Wamejenga hoja wengi katika Maimamu kama vile Al-Zuhry na Al-Shaafiy kupitia Ayah hii Tukufu juu ya kwamba matendo ni katika Iymān.
 
 
Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Sharh Hadith Jibriil