43.Faida Katika Hadithi Ya Jibriil – 38


Yatano:

Swaum ya Ramadhani ni Ibada ya kiwiliwili, nayo ni siri iliyopo baina ya mja na Mola wake, hakuna anayemuona isipokuwa Allāh Subhānah Wata’aala. Kwa sababu hupatikana baadhi ya watu wanaokula mchana wa Ramadhani na wengine wanawadhania kuwa wamefunga. Na huenda mmoja wao akawa amefunga swaum ya sunnah na mwenzake akadhani kuwa ni mwenyekula. Na kwaajili ya hili imekuja hadithi sahihi kwamba mtu atalipwa kwa amali yake jema moja kwa kumi mfano wake, mpaka nyongeza mia saba. Amesema Allāh ‘Azza wajalla-:
“Isipokuwa Swaum kwani hiyo ni yangu Mimi, na Mimi ndiye ninayelipa”.
Ameipokea Bukhari (1894), na Muslim (164).
Yaani: Atalipa bila ya hesabu.
Na matendo yote (ya Kiibada) ni ya Allāh ‘-Azza wajalla-:
Kama alivyosema ‘Azza wajalla-:

“قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ” الأنعام (١٦٢)
لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ” (١٦٣)

“Sema: Hakika ya Swala zangu na Vichinjwa vyangu na Mema niyatendayo kwenye uhai wangu, na Mema baada ya kufa kwangu, vyote hivyo ni vya Allāh Mola wa Walimwengu wote.
Hana mshirika, na kwa hilo (la Ikhlās) nimeamrishwa, na Mimi ni Muislam wa kwanza (katika Umma huu)”.
Al-An-Aam (162-163).
Na hakika imehusishwa Swaum katika hii Hadithi kuwa ni ya Allāh, kwa sababu ya ile hali ya kificho iliopo katika hii Ibada, na kwamba hakuna anayeiona zaidi ya Allāh.
 
Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Sharh Hadith Jibriil