01.Utangulizi


بسم الله الرحمن الرحيم

الحمد لله رب العالمين، والصلاة والسلام على نبينا محمد وعلى آله وأصحابه إجمعين، والتابعين لهم بإحسان إلى يوم الدين

أما بعد

Hakika miongoni mwa neema za Allāh Mtukufu juu ya Ummah huu, ni kuupa Wanazuoni wachamungu, ambao wamesimama kwa lengo la kuudifai Uislamu na kuutetea, na wakasimama dhidi ya maadui wake na kuwatahadharisha, na wakalingania katika kufuata Kitabu na Sunnah.
Na miongoni mwa hao Wanazuoni wakubwa ni Shaykhul-Islām Abiyl-‘Abbās Ahmad bin Taymiyyah (Allāh amraham).
Kwa hakika alipambana katika njia ya Allāh kwa bayana na silaha, na vitabu vyake vilikuwa na athari kubwa sana na manufaa, hivyo kwa haki kabisa vilistahiki kuitwa “Hidaya kwa waliobaki njia panda” na “Uokozi kwa anayekufamaji” na “Mwangaza njiani”, bali ni marejeo ya kila mwenye kushikamana na Kitabu na Sunnah, na ndio maana wamevipa umuhimu mkubwa Wanazuoni na wanafunzi wao, na wakavitia maanani sana.
Kama ambavyo hata Wafalme katika miji hii (Allāh aihifadhi) wamevichukulia kwa umuhimu mkubwa sana, kwa namna ya kwamba wameamrisha vichapishwe na vigawiwe vitabu vya Shaykhul-Islām (Allāh amraham), kwa hakika aliamrisha Mfalme ‘Abdul-‘Aziiz (Allāh amraham) vichapishwe na kugawiwa (kwa watu), na wamemfuatia katika hilo watoto wake (Allāh awape tawfiiq na awabariki, na awarehemu waliokufa miongoni mwao).
Kama ambavyo kwamba Mufty aliyepita Shaykh Muhammad bin Ibrahim, na Mufty ‘Abdul-‘Aziz bin Bāz walikuwa wakivijali mno, kadhalika na wengineo (Allāh awarehemu kwa rahma zake pana).
Na awaafikishe Viongozi wetu katika yale anayoyapenda na kuyaridhia.
Na kwa hakika nimependa kushiriki katika kupata ujira na kuwanufaisha Waislamu kwa yale ambayo yamekuwa rahisi (kwangu) kutokana na majibu na fatawa za Shaykhul-Islām, nikaonelea niweke maswali kisha ninakili jawabu la Shaykhul-Islām kwa maandiko yake pasi na kuziongeza au kuzidisha.
Allāh amraham Shaykhul-Islām Ibn Taymiyyah na amghufirie!
Na amlipe kutokana na Uislamu na Waislamu jaza ya kheri!
Na amlipe maradufu yule atakayechapisha na kusambaza vitabu vyake na kuvigawa kwa lengo la kutarajia thawabu za Allāh mwenye Izza na Utukufu.
 
 
 
Muhusika: Shariif bin Aliyy Al-Raajihiy
Kiunganishi: http://duaatsalaftz.net/category/makala/kumwokoa-mfamaji/
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Ighāthatul-Ghariiq
Imehaririwa: 11 Swaffar/1441H