02.Kumwokoa Mfamaji na Kuangaza Njia


1- Ni upi msimamo wa Ahlus-Sunnah juu ya Maswahaba (Allāh awaridhie)??
Jibu- Miongoni mwa misingi ya Ahlus-Sunnah Wal-Jama’ah ni kusalimika kwa mioyo yao na ndimi zao kwa Maswaba wa Mtume wa Allāh ﷺ, kama alivyowasifu Allāh kwa hilo katika kauli yake Mtukufu:

“وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ    ” الحشر (١٠)

“Na waliokuja baada yao wanasema: “Ewe Mola wetu! Tusamehe sisi na ndugu zetu waliotutangulia (kufa) katika Uislamu. Wala Usijaalie katika nyoyo zetu undani kuwafanyia Waislamu (wenzetu). Mola wetu! Hakika Wewe ni Mpole Mwingi wa rehema”.
Al-Hashr (10).
 
 
Muhusika: Ibn Taymiyyah Al-Harrāniy
Kiunganishi: http://duaatsalaftz.net/category/makala/kumwokoa-mfamaji/
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Al-Wāsitwiyyah Uk. 184
Imehaririwa: 11 Swaffar/1441H