03.Kumwokoa Mfamaji na Kuangaza Njia


2- Ni upi msimamo wa Ahlus-Sunnah juu ya Watu wa nyumba ya Mtume ﷺ (Ahlul-Bayt)??

 

Jibu- Wanawapenda watu wa nyumba ya Mtume wa Allāh ﷺ, na kuwatetea, wanawahifadhia wosia wa Mtume wa Allāh ﷺ, pale aliposema siku ya Ghadiir Khum:

“أذكركم الله في أهل بيتي”

“Nakukumbusheni (kwa jina la) Allāh kuhusu watu wa nyumbani kwangu”.
Ameipokea Muslim(2408). Hadithi ya Zayd bin Arqam (Allāh amridhie).
Na akasema tena kumwambia ammy yake Al-‘Abbās (Allāh amridhie), baada ya kuwa alimshatakia kwamba baadhi ya Quraysh wanawatazama vibaya baniy Haashim, akasema:

“والذي نفسي بيده لا يؤمنون حتى يحبوكم لله ولقرابتي”

“Naapa kwa ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake! Hawawezi wakawa waumini (wakamilifu wa imani) mpaka wakupendeni nyinyi kwa ajili ya Allāh na udugu wangu”.
Ameipokea Ahmad (1777). Hadithi ya ‘Abdul-Muttwalib bin Rabii’ah (Allāh amridhie).
 
 
 
Muhusika: Ibn Taymiyyah Al-Harrāniy
Kiunganishi: http://duaatsalaftz.net/category/makala/kumwokoa-mfamaji/
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Al-Wāsitwiyyah Uk. 195
Imehaririwa: 11 Swaffar/1441H