04.Kumwokoa Mfamaji na Kuangaza Njia


3- Ni upi msimamo wa Ahlus-Sunnah juu ya wake wa Mtume ﷺ??
Jibu- Wanawapenda na kuwatetea wake wa Mtume ﷺ, ambao ni mama wa Waislamu, na wanaamini kuwa wao ni wake zake pia akhera, hasa hasa Khadija (Allāh amridhie), mama wa watoto wake wengi, na wa kwanza kumwamini na kuungana naye katika jambo lake, na alikuwa ana nafasi kubwa sana kwake.
Pia Swiddiiqah mwana wa Swiddiiq (Allāh amridhie).
Kuhusu yeye amesema Mtume ﷺ:

“فضل عائشة على النساء كفضل الثريد على سائر الطعام”

“Ubora wa Aisha juu ya wanawake wengine ni ubora wa tharidi mbele ya vyakula vingine”.
Ameipokea Bukhari. Hadithi ya Abū Mussa Al-Ash-‘Ariyy (Allāh amridhie).
 
 
 
Muhusika: Ibn Taymiyyah Al-Harrāniy
Kiunganishi: http://duaatsalaftz.net/category/makala/kumwokoa-mfamaji/
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Al-Wāsitwiyyah Uk. 198
Imehaririwa: 11 Swaffar/1441H