07.Kumwokoa Mfamaji na Kuangaza Njia


6- Ni upi msingi wa (Dini ya) Raafidhwah?
Jibu- Msingi wa (Dini ya) Raafidhwah (shia) ni: Kwamba Mtume ﷺ , alitoa maelekezo ya wazi juu ya ‘Aliyy (Allāh amridhie), yenye Kukata udhuru, na kwamba yeye (‘Aliyy) ndiye Kiongozi asiyekosea (Ma’sum), na atakayekwenda naye kinyume amekufuru.
Na kwamba (Maswahaba) Muhājiriina na Answār (Allāh awaridhie), waliyaficha maelekezo ya uteuzi (wa Mtume ﷺ), na wakamkana Imam asiyekosea, na wakafuata matamanio ya nafsi zao, na wakayabadilisha (mafunzo ya) Dini, na wakaigeuza Shari’ah, na wakafanya dhulma na uadui(mkubwa)!, bali wakakufuru ila wachache tu (miongoni mwao), watu kumi na watatu au zaidi yao (kidogo)!.
Kisha wanasema:
“Hakika Abūbakar na ‘Umar na mfano wao waliendelea kuwa ni wanafiki”.
Na huenda ukawaona wanasema:
“waliamini kisha wakakufuru”.
Na wengi wao wanawakufurisha (wale) wote wanaokwenda kinyume nao. Na wanajiita wao ndio Waumini, na wanaowakhalifu wao ni makafiri.
 
 
 
Muhusika: Ibn Taymiyyah Al-Harrāniy
Kiunganishi: http://duaatsalaftz.net/category/makala/kumwokoa-mfamaji/
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Majmu’u Fatāwaa Jz 3, S 356.
Imehaririwa: 12 Swaffar/1441H