08.Kumwokoa Mfamaji na Kuangaza Njia


7- Ni yapi wayafanyayo Rāfidhwah zinapogongana kwao kauli mbili?
        Jibu- Nimeona kundi la masheikh wa Rāfidhwah (shia) kama vile Ibn Al-‘Uud Al-Hilliy asemaye:
“Wanapotofautiana (shia) imaamiyyah juu ya kauli mbili, moja ya kauli hizo anajulikana msemaji wake, na nyingine hajulikani msemaji wake, basi kauli hiyo ambayo hajulikani msemaji wake ndio kauli ya haki ambayo ni wajibu kuifuata, kwa sababu (Imam) anayesubiriwa ujio wake asiyekosea yupo kwenye fungu hilo”.
Na huu ni ujinga na upotevu uliopea ,kwani kwa hali ya kukadiria uwepo wa huyo (Imam) anayengojewa ambaye hakosei, bado hatutokuwa na yakini kuwa ameyasema hayo (au hakuyasema), kwakuwa hakuna mmoja aliyenukuu hilo kutoka kwake, wala kutoka kwa aliyenukuu kutoka kwake, sasa kipi kimempa ujasiri wa kukata kauli kuwa (hiyo kauli ya asiyejulikana) ni kauli yake?
Na kipi kinachozuia kauli ile nyingine isiwe kauli yake?
Na yeye kuwepo kwake ughaibuni na kuwakhofia kwake madhalimu hatoweza kudhihirisha kauli yake, kama wanavyodai wenyewe.
Hivyo msingi wa Dini wa hawa Răfidhwah umejengeka juu ya (mtu) asiyejulikana ambaye hayupo. Na wala msingi wa Dini yao haukujengwa kwa ambacho kipo chenye kueleweka.
Wanadhani kwamba Imam wao yupo na amekingwa na makosa, ilhali ameadimika wala hayupo.
Na laiti angelikuwa yupo na amekingwa na makosa, bado watabaki kuwa hawana wajualo kuhusu yeye, si kwa amri zake wala makatazo yake, kama walivyokuwa wakijua amri na makatazo ya wazi wake (kabla yake).
 
 
 
Muhusika: Ibn Taymiyyah Al-Harrāniy
Kiunganishi: http://duaatsalaftz.net/category/makala/kumwokoa-mfamaji/
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Minhaaj Jz 1, S 89-90
Imehaririwa: 12 Swaffar/1441H