11.Kumwokoa Mfamaji na Kuangaza Njia


10- Ni juu ya msingi gani hujengeka ushirkina na uzushi?
            Jibu- Shirki na bidaa zote hujengeka juu ya msingi wa uongo na uzushi. Na kwa mantiki hii, kila atakayejiweka mbali na Tawhiid na Sunnah, atakuwa na ukaribu zaidi na ushirikina na uzushi.
Kama vile Rāfidhwah (shia), ambao ni waongo wakubwa kuliko warongo wote, na ni washirikina mno, hakuna katika watu wanaoendekeza matamanio ya nafsi zao waongo wakubwa kama wao, wala wale watakaokuwa mbali na Tawhiid wakawashinda wao.
Ndio maana wanaiharibu Misikiti ya Allāh ambayo hutajwa ndani yake jina lake, wanaiharibu na kuikosesha Jamaa na Ijumaa, na wanaimarisha majengo ya makaburi ambayo Allāh na Mtume wake wamekataza yasijengwe.
Allāh Mwenye Utakasifu ameamuru katika Kitabu chake iimarishwe Misikiti sio makaburi.
 
 
Muhusika: Ibn Taymiyyah Al-Harrāniy
Kiunganishi: http://duaatsalaftz.net/category/makala/kumwokoa-mfamaji/
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Iqtidhaa Jz 2, S 759-760.
Imehaririwa: 25 ‘Rabiul 1/1441H