46.Faida Katika Hadithi ya Jibriil – 41


Yanane:

Kauli yake aliposema: “Umesema kweli!
Akasema (Umar): “Tukamstaajabu, anamuuliza kisha anamsadikisha!”.
Wajihi wa kustaajabu ni kuwa aghlabu [1] muulizaji huwa hajui jawabu, hivyo huwa anauliza ili apate kujua. Na mtu kama huyu haitakikani kumwambia yule aliyemuuliza kuwa “Umepatia, au umesema kweli”, kwa sababu huyu muulizaji akiyasema haya itajulikana kuwa alikuwa analo jawabu. Na ndio maana wakastaajabu Maswahaba kutokana na uswadikishaji huu kutoka kwa muulizaji huyu aliye mgeni.

 

———————
[1] Yaani: Mara nyingi, kinyume na wale ambao wanalikengeusha neno hilo kulitoa katika maana yake.

 

 

Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Sharh Hadith Jibriil