47.Faida Katika Hadithi ya Jibriil – 42


Kauli yake (Jibriil), aliposema: “Nihabarishe kuhusiana na Iymān”.
Akasema (swalla Llāhu’alayhi wasallam): “Ni kumuamini Allāh, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, na kuamini Qadar, kheri zake na shari zake”.
Akasema (Jibriil): “Umesema kweli. Kisha akasema: Nihabarishe kuhusiana na Ihsān”.
Akasema (Mtume swalla Llāhu’alayhi wasallam): “Ni wewe kumuabudu Allāh kana kwamba unamuona. Na ukiwa humuoni basi (fahamu) kuwa yeye anakuona”.
Katika kipengele hiki kuna faida nyingi.

Ya kwanza:

Jawabu hili limekusanya nguzo za Iymān ambazo ni sita. Na ya kwanza kabisa ni kumuamini Allāh, nayo ni nguzo kuu kwa kila ambacho kinatakikana kuaminiwa (basi nguzo hii ni asasi yake), na ndio maana ikaegemezwa juu yake (Iymān) ya kuamini Malaika, Vitabu, Mitume nk. Na asiyemwamini Allāh hawezi kuamini zilizobaki katika nguzo (za Iymān).
Na kumwamini Allāh kuna kusanya kuamini juu uwepo wake, na Ruubuubiyya, Uluuhiiyyah, Majina na Sifa zake.
Na kwamba yeye Allāh Subhānah Wata’aala ni mwenye kusifika kwa kila sifa yenye ukamilifu inayoendana na yeye, pia ametakasika kutokana na kila sifa zenye mapungufu.
Hivyo ni wajibu kumpwekesha katika Rubuubiyyah, Uluuhiiyyah, Majina na sifa zake.

 

 

Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Sharh Hadith Jibriil