50.Faida Katika Hadith ya Jibriil – 45


Ya kwanza (ث):

Mgawanyo huu wa Tawhiid umejulikana kwa kuzisoma nususi za Kitabu na Sunnah [1], na limekaa wazi hilo kwa ile sura ya kwanza katika Qur’an, pamoja na sura ya mwisho. Kwani zote hizo mbili zimetaja aina tatu za Tawhiid.
Ama Suratul-Fātiha, hakika ayah yake ya kwanza ambayo ni:
“الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ” (2)
“Sifa zote njema anastahiki Allāh Mola wa Walimwengu wote”.
Al-Fātiha (2).
Hakina neno الْحَمْدُ لِلَّهِ ndani yake kuna Tawhiidul-Uluuhiyyah. Kwa sababu tendo la kuegemeza himdi na shukrani kwake yeye (Allāh), kutoka kwa waja wake hiyo imetosha kuwa ni Ibada.
Na katika kauli yake رَبِّ الْعَالَمِينَ ndani yake kuna kuthibitisha Tawhiidul-Rubūbiyyah. Ambayo ina maana ya kuwa Allāh ‘Azza Wajalla- ndiye Mola Mlezi wa Walimwengu wote. Na Walimwengu ni kila asiyekuwa Allāh, kwani hakuna katika vilivyopo zaidi ya Muumba na viumbwa, na Allāh ndiye Muumba, na kila asiyekuwa yeye ni muumbwa. Na miongoni mwa majina ya Allāh ni “Arrabbu” [3], na kabla ya jina hili kuna jina الله, katika ayah hii hii.
———————–
[1] Kama walivyosoma Wanavyuoni katika Kitabu na Sunnah wakatutolea shuruti za swala na vinginevyo.
[2] Sheikh (Allāh amhifadhi) amepita katika mapito ya kuwa “Bismillāh” si ayah katika Al-Fātiha. Na masuala haya yameleta ikhtilafu kubwa sana baina ya Wanavyuoni wetu baina ya walioizingatia kuwa si ayah katika sura yoyote. Na hii rai ya Imam Mālik, Al-Awzaa’iy, Abū Haniifah, na Imam Daud. Na wana hoja zao.
Na waliokwenda kimadhehebu kuwa ni ayah katika Al-Fātiha na katika kila sura. Na hii ni rai ya Imam Shaafiy, Ahmad, Is-Haaq, na Abū Ubayd. Na wana zao hoja.
[3] Kwa maana: hii ni dalili ya aina ya tatu ya Tawhiid, ambayo ni Tawhiid ya Majina na Sifa.

 

 

Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Sharh Hadith Jibriil