51.Faida Katika Hadithi ya Jibriil – 46


Ya kwanza (ج):

Na kauli yake:
الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Imebeba aina ya Tawhiidil-Asmaa Wasswifāt. Na neno “Al-Rahmān” na “Al-Rahiim” , ni majina mawili miongoni mwa majina ya Allāh, yanajulisha juu ya sifa miongoni mwa sifa za Allāh, nayo ni sifa ya “Huruma”.
Na majina ya Allāh yote ni majina yanayotolewa ndani yake sifa, hakuna jina ambalo ni “Jāmid” lisilobeba sifa fulani. Bali kila jina miongoni mwa majina ya Allāh limebeba sifa miongoni mwa sifa zake [1].
———————
[1] Mfano jina “Al-Tawwāb”, ni jina lake, na limebeba sifa ya kukubali toba kutoka kwa waja wake. Ukilijuwa hilo, juwa pia kuna pote potovu linalomthibitishia Allāh majina yake pasi na sifa katika majina hayo.

 

 

Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Sharh Hadith Jibriil