52.Faida Katika Hadithi ya Jibriil – 47


Ya kwanza (ح):

Na
مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ” (4)”
“Mwenyekumiliki siku ya Malipo”.
Ndani yake ayah hii kuna kuthibitisha Tawhiidir-Rubūbiyyah.
Na ni yeye (Allāh) Subhānah ndiye mwenye kumiliki dunia na akhera. Lakini hapa imetajwa kuwa yeye ndiye Mwenye kumiliki siku ya malipo, kwa sababu siku hiyo viumbe wote watanyenyekea kwa Mola wa Walimwengu wote. Kinyume na duniani, walishapatikana waliochupa mipaka na kufanya kiburi, na (miongoni mwao alisema):
“أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ  ” النازعات( ٢٤)
“Mimi ndiye Mola wenu niliyetukuka zaidi (niliyejuu)”.
An-Nāziaat (24).

 

Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Sharh Hadith Jibriil