53.Faida Katika Hadithi ya Jibriil – 48


Ya kwanza (خ):

Na kauli yake:

“إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ  ” الفاتحة (٥)

“Wewe tu ndiye tunayekuabudu. Na wewe tu ndiye tunayekuomba msaada”.
Al-Fātiha (5).
Ayah hii ndani yake kuna uthibitisho wa Tawhiidul-Ulūhiyyah.
Na kutangulizwa kwa mtendwa “مفعول” ambaye ni neno (إياك), hufidisha kudhibiti na kuibana (Ibada). Na maana yake itakuwa: Tunaihusisha kwako wewe tu Ibada na kuomba msaada. Na wala hatutomshirikisha pamoja nawe yeyote [1].
—————–
[1] Na hii ndiyo maana ya Tawhiidil-Uluuhiyyah.

 

Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Sharh Hadith Jibriil