54.Faida Katika Hadithi ya Jibriil – 49


Ya kwanza (د):

Na kauli yake:

“اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ (٦). صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ ” الفاتحة (٧)

“Tuongoze njia iliyonyooka. Njia ya wale ulioneemesha juu yao. Si njia ya wale uliowaghadhibikia wala waliopotea”.
Al-Fātiha (6-7).
Ndani yake hupatikana Tawhiidul-Ulūhiyyah, kwa sababu kumuomba Allāh Uongofu “Hidāyah” ni Dua. Na alishasema Mtume (swalla Llāhu’alayhi wasallam):

“الدعاء هو العبادة”

“Ibada ni Dua”.
Hivyo mja anamuomba Mola wake katika
Dua hii, amuongoze njia iliyonyooka, ambayo imepitwa na Manabii, na Siddiiquun, Mashahidi pamoja na Waja wema, ambao ndio watu wa Tawhiid. Na wakati huo huo anamuomba amuepushe kutokana na njia ya walioghadhibikiwa juu yao, pamoja na waliopotea. Ambao imekosekana kwao Tawhiid. Bali kilichopatika kutoka kwao ni ushirikina na kumuabudu asiyekuwa Yeye.

 

 

Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Sharh Hadith Jibriil