55.Faida Katika Hadithi ya Jibriil – 50


Ya kwanza (ذ):

Ama kuhusu Sūratun-Nās, kauli yake:

“قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ  ” الناس (١)

“Sema najikinga kwa Mola wa watu”.
An-Naas (1).
Kuna uthibitisho wa aina tatu za Tawhiid. Kwani hakika kuomba kinga kutoka kwa Allāh hili hupatikana ndani yake Tawhiidil-Uluuhiyyah.
Na neno: بِرَبِّ النَّاسِ kuna uthibitisho wa Tawhiidir-Rubūbiyyah pamoja na Tawhiidul-Asmaai Wasswifāt. Na ayaha hii ni sawa na ayah isemayo [1]:

“الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ  ” الفاتحة (٢)

“Sifa zote njema anastahiki Allāh Mola wa Walimwengu wote”.
Al-Fātiha (2).
——————-
[1] Kwa maana ya kuwa zote mbili zimekusanya aina zote tatu za Tawhiid.
 
 
 
Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-‘Abbād
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Sharh Hadith Jibriil