56.Faida Katika Hadithi ya Jibriil – 51


Ya kwanza (ر):

Kauli yake: (٢) (مَلِكِ النَّاسِ)
“Mfalme wa watu” (2).
Ndani yake kuna uthibitisho wa Tawhiidir-Rubūbiyyah pamoja na Tawhiidil-Asmaa Wasswifāt.
Na neno: (٣) (إِلَٰهِ النَّاسِ)
“Muabudiwa wa watu”. (3).
Ndani yake kuna uthibitisho wa Tawhiidil-Ulūhiyyah pamoja na Asmaa Wasswifāt.
Na mnasaba uliopo baina ya aina tatu hizi za Tawhiid, ni kwamba Tawhiidur-Rubūbiyyah na Tawhiidul-Asmaai Wasswifāt, hizi mbili zinalazimisha kupatikana kwa Tawhiidul-Ulūhiyyah. Na Tawhiidul-Ulūhiyyah inadhamini uwepo wa aina mbili hizo.
Kwa maana: Yeyote atakayekiri juu ya Tawhiidil-Ulūhiyyah, hakika atakuwa amekiri pia Tawhiidir-Rubūbiyyah na Tawhiidil-Asmaa Wasswifāt. Kwa sababu atakayekiri na kukubali kuwa Allāh pekee ndiye Muabudiwa, na akamhusisha kwa Ibada peke yake, na wala hakumjaalia mshirika katika hizo Ibada [1], bila shaka hatokuwa ni mpingaji juu ya kuwa Allāh yeye ndiye Muumba, Mwenye kuruzuku, Mwenye kuhuyisha, Mwenye kufisha [2], na kwamba Majina mazuri sana ni yake yeye na sifa zilizojuu ni zake [3].
——————–
[1] Na hii ndiyo inayoitwa Tawhiidul-Ulūhiyyah.
[2] Na hii ndiyo inayoitwa Tawhiidur-Rubūbiyyah.
[3] Na hii ni Tawhiidul-Asmaai Wasswifāt.

 

 

Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Sharh Hadith Jibriil