Hukmu ya kufunga ndoa na mjamzito


Swali:
Assalamu aleykum warahmatullah Wabarakaatuh
Naomba kuuliza kuhusu hukmu ya ndoa na mwanamke ambaye ni mjamzito.
Jibu:

وعليكم السلام ورحمة الله وبركاته
الحمد لله رب العالمين والصلاة والسلام على رسول الله صلى الله عليه وسلم

Ndugu muulizaji:
Suala la kufunga ndoa na mwanamke ambaye ni mjamzito ( mwenye mimba ) ni jambo lisilo kubalika kisheria.
Na hilo ni kwa Dalili zifuatazo:-
Hadithi ya kwanza:-

عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه قال أن النبي صلى الله عليه وسلم قال في سباياأوطاس: لا توطأ حامل حتى تضع ، ولا غير ذات حمل حتى تحيض حيضة
{ رواه أبو داود1257 ، ألحاكم 2/212,وإسناده حسن )

Imesimuliwa kutoka Abu Saidy Khudriy Allah amridhie amesema:
Hakika Mtume صلى الله عليه وسلم amesema kuhusu mateka wa kike wa huko Awtwaasi;
Haingiliwi mjamzito mpaka azae hata mwanamke mwingine mjamzito haingiliwi mpaka apate hedhi
(Abuu Daudi 1257,Alhaakimu 2/212)
Hadithi ya pili:-

عَنْ رُوَيْفِعِ بْنِ ثَابِتٍ الْأَنْصَارِيِّ، قَالَ: قَامَ فِينَا خَطِيبًا، قَالَ: أَمَا إِنِّي لَا أَقُولُ لَكُمْ إِلَّا مَا سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ َيقُولُ: يَوْمَ حُنَيْنٍ، قَالَ لَا يَحِلُّ لِامْرِئٍ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ أَنْ يَسْقِيَ مَاءَهُ زَرْعَ غَيْرِه

(.رواه أبوداود 2158 وصححه الألباني ).

Amesimulia Ruwayfii lbnu Thaabiti Al-answaariy amesema, alisimama mbele yetu Khatwibu akasema, Ama mimi sisemi kwenu ila kile nilicho msikia Mtume صلى الله عليه وسلم anasema siku ya Hunayni akasema,
Haimpasi mtu mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho amwage maji (ya uzazi / manii ) juu ya mbegu aliyo iotesha mwingine {mwanamke ni mjamzito}
(Abuu Daudi 2158, Imesahihishwa na Sheikh Albany Allah amrahamu ).
Hadith ya tatu :-

عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ فِي غَزْوَةٍ فَرَأَى امْرَأَةً مُجِحًّا فَقَالَ:»لَعَلَّ صَاحِبَهَا أَلَمَّ بِهَا؟« قَالُوا: نَعَمْ، فَقَالَ: »لَقَدْ هَمَمْتُ أَنْ أَلْعَنَهُ لَعْنَةً تَدْخُلُ مَعَهُ فِي قَبْرِهِ، كَيْفَ يُوَرِّثُهُ وَهُوَ لَا يَحِلُّ لَهُ؟ وَكَيْفَ يَسْتَخْدِمُهُ وَهُوَ لَا يَحِلُّ لَهُ؟

(رواه أبو داود 2156).

Amesimulia Abuu Dardai, Hakika Mtume wa Allah صلى الله عليه وسلم alikua vitani akamuona mwanamke mjamzito anaekaribia kujifungua (mlangoni kwa mtu) akauliza “Huenda amemjia mtu wake (kwa lengo la kujamiiana”?) Wakasema ndiyo, akasema hakika nilikusudia kumlaani huyo mwanaume laana ambayo ingeingia (hiyo laana) pamoja nae kaburini mwake, vipi atamrithi na yeye siyo halali yake? na vipi atamuhudumia na yeye siyo halali yake?
(Abuu Daudi 2156).
Hadithi ya nne :-

عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّب ِأَنَّ رَجُلًا تَزَوَّجَ امْرَأَةً فَلَمَّاأَصَابَهَا وَجَدَهَا حُبْلَى فَرَفَعَ ذَلِكَ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم, َ فَفَرَّقَ بَيْنَهُمَا وَجَعَلَ لَهَا الصَّدَاقَ وَجَلَدَهَا مِائَة

( سنن سعيد إبن منصور671)

Amesimulia Saidy lbnu Musayyibi, Hakika kuna mtu alioa mwanamke, basi alipo muingilia akamkuta mjamzito, akashtakia jambo hilo kwa Mtume صلى الله عليه وسلم , basi akawatenganisha wawili hao na akamwachia mahari yake na akampiga mijeledi mia moja
(Sunanu Saidy lbnu Manswuur 671).
Ndugu muulizaji:
Katika hadithi tulizo zileta huko nyuma Kuna mambo muhimu tunajifunza. Miongoni mwa mambo hayo ni kuwa :-
  1 Ni haramu kumuingilia mwanamke ambaye ni mjamzito ( mwenye mimba ) kwa Hali yeyote ile
Na kutokana na jambo hilo mtume صلى الله عليه وسلم alidhamiria kumlani mtu kwasababu hio.
  2 Ndoa iliyofungwa Hali yakuwa mwanamke ni mjamzito ni batili
Hilo linaonekana pale mtume صلى الله عليه وسلم alipoletewa mashtaka juu ya kadhia hii na akawatenganisha wahusika

لا يجوز نكاحها قبل وضع الحمل لا من الزاني نفسه ولا من غيره وهو مذهب المالكية والحنابلة وأبي يوسف من الحنفية, واشترط الحنابلة لجواز نكاح الحامل بعد وضع حملها التوبة من الزنى

Haifai kumuoa mjamzito kabla ya kujifungua iwe muoaji amezini nae au muolewaji amezini na mtu mwingine nao ndiyo msimamo wa madhehebu ya Maliki na Hanafi na Abuu Yuusufu katika Mahanafi, wakaweka sharti Mahambaliy kumuoa mjamzito baada ya kujifungua ni (lazima) atubu kutokana na zinaa.

​​قال شيخ الإسلام​​

Ndoa ya mzinifu ni haramu ​​mpaka atakapotubia​​ , sawa iwe ( uyo anaetaka kumuoa ) ndie aliezini nae au mwengine , na hili ndilo sahihi bila shaka …
Madhehebu ya Imam Hanbal nao wanajuzisha ndoa ya wazinifu kwa masharti mawili nayo ni kutubia waliozini na kumalizika eda yake mwanamke ,:-
“ Na ni haramu kwa mzinifu mwanamke kuolewa na mzinifu mwanamme ( aliyezini na mwengine ) hadi atubie huyo mwanamke na amalize eda yake .”
( tazama Rawdhul Murabbai juzuu 3 uk 83 .)
“ Na wanavyuoni wamekhitilafiana kuhusu kujuzu kumuoa mwanamke mzinifu kabla ya kutubia kwake katika kauli mbili mashuhuri , lakini Quraan na Hadithi na mazingatio yanajuulisha kuwa ndoa hiyo haijuzu ( kabla ya kutubia ) .”
( tazama Majmuu Fatawa Ibnu Taymiya juzuu 32 uk 145 ,na katangulia maneno mfano wa haya uk 141.)
Na ndiyo msimamo wa Jumhuri.
Katika zama hizi nyingi katika familia zinajiingiza katika makosa haya kwa kutaka kujisitiri kutokana na aibu hiyo hali ya kuwa wanamkosea muumba wao.
Ewe mzazi mtunze binti yako na harakisha kumuoza pindi anapokujieni kijana aliyetimiza vigezo vilivyowekwa na uislamu
Kinyume na hayo utapatikana ufisadi wa wazi katika ardhi.
Ewe kijana chunga mwenendo wako na hifadhi tupu yako.
Ikitokea haja fanya hima kuoa kwani ndiyo salama yako katika Dunia yako na Akhera yako.
Na Allah Tabaaraka Wata’aala ni mjuzi zaidi.
Mhusika : duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 7’J-Uwlaa/1439.