Hukmu Ya Kuimba Wimbo Wa Taifa Na Kusimama Wakati Wa Bendera Kupandishwa Na Kushushwa


Swali:
Mimi ni mwanafunzi wa shule ya serikali kila kila huimba wimbo wa taifa pia ni lazima kusimama ikishushwa au ikipandishwa hili suala kama muislamu ni ipi hukumu yake ?
Jawabu:
الحمد لله رب العالمين والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء وإمام المرسلين
وبعد.
Swali kama hili liliwahi kuulizwa kwenye “Al-Lanatid-Daaimah” kamati ya kudumu ya kutoa fat’wa katika nchi ya Hijazi (Saudia) fat’wah No 5963:
Na majawabu yao yalikuwa kama ifuatavyo.
“Haijuzu kuisalimu bendera (kuisimamia ishara ya salamu) bali jambo hilo ni bid’ah iliyozushwa. Na amesema Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) :
”Yeyote atakayezuwa katika jambo letu hili (La Dini) kile ambacho hakimo basi atarudishiwa” Bukhariy 2697 na Muslim 171.
Ama suala la kuwaheshimu maafisa (wa jeshi) na kuwaweka kwenye nafasi zao (kiheshima) ni jambo lenye kujuzu ila tu kuchupa mipaka katika hilo ni jambo lisilofaa wawe ni maafisa au wasiwe maafisa”.
Na iliwahi pia kuulizwa “Al-Lajnah” fat’wa No 2123:
“Je inafaa kusimama kwa kiheshima na kuadhimisha salamu zozote za Kinchi au kwajili ya bendera ya Nchi!?

Jawabu:

Haijuzu kwa Muislam kusimama kwa taadhima bendera yoyote ya Nchi au salamu yoyote ya Kinchi. Bali mambo hayo ni miongoni mwa Uzushi mkubwa ambao haujawahi kuepo wakati wa Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) wala wakati wa Makhalifa wake waongofu (Allaah Awaridhi!)
Na tendo kama hilo linakinzana na ukamilifu wa Tawhiidi ya wajibu na kumtakasia Allaah Ta’dhiima na kumtukuza.
Bali ni njia ipelekeayo kwenye ushirikina. Na ndani yake kunakujishabihisha na makafiri na kuwaiga kwenye ada zao chafu. Na kujikomba nao katika hali ya kupetuka mipaka kwa viongozi wao na rasimu zao.
Na ametukataza Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) kutokana na kujifananisha nao.
Wabillaa Al-Tawfiiiq”.
Huenda kajiuliza muulizaji wa nafsi yake ya kuwa
“Mbona tumeambiwa kuwa tunatakiwa tuitii dola! Na kuiheshimu bendera si ni katika kuiheshimu Dola!?
Jawabu analitoa Al-Imaam Al-Fawzaan (Allaah Amhifadhi!):
“Salamu huwa baina ya Waislamu, na haiwi salamu kwa vitu jamaadaat (kama vile nyumba , jiwe, dirisha , kitambaa nk.) na vitambaa na mfano wake.
Kwasababu (salamu) ni Dua ya kuomba salama kutokana na maafa. Au ni jina miongoni mwa majina ya Allaah. Ataomba Muislamu kupitia jina hilo kumuombea nduguye Muislamu ili apate baraka na kheri za jina hilo (la Allaah, kwa kusema assalaam ‘alaykum) na mudari wa salamu kwa bendera ni kuisimamia kwa kuitukuza na kuioneshea taadhima….
Tunasema, Tunaiheshimu Serekali kwa lile ambalo limeweka na Shari’ah ya Allaah (kwetu sisi), kuwa ni wasikivu na watiifu kwa mambo ya wema na pia kuwaombea (viongozi wetu) Tawfiiq”
Jarida la Al-Jaziirah No 1198.
Kwa hayo tumeona kuwa haifai kuisimamia bendera wala haifai kumsimamia Mtu kwa lengo la kumtukuza na kumuadhimisha.
Sana sana kusimama kwa lengo la kumlaki mgeni.
Ama kusimama kwa dhamira ya heshima na ihtiraamu kwa usmimamiae haifai hata kama ni mwalimu au Shaykh.
Na usighurike na maneno ya Ahmad Shawqiyy (Mshairi wa Misr) aliyesema:

قم للمعلم وفه التبجيلا**
كاد المعلم أن يكون رسولا.
أعلمت أشرف أو أجل من الذي**
يبني وينشئ أنفسا وعقولا.
سبحناك اللهم خير معلم**
علمت بالقلم القرون الأولى .
Kwani hayo aliyoyasema yanapishana na mafunzo ya Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam),
“Yeyote atakayependa kusimamiwa basi ajiandalie makazi yake motoni”.
na pia al-hamdulillaah alijibiwa na Ibraahim Twuuqan akasema:
(شوقي) يقول- وما درى بمصيبتي-
“قم للمعلم وفه التبجيلا”
أقعد-فديتك, هل يكون مبجلا
من كان للنشئ الصغار خليلا..!؟
وكاد (يفلقني ) الأمير بقوله..
كاد المعلم أن يكون رسولا…!
لو جرب التعليم (شوقي) ساعة
لقضى الحياة شقاوة وخمولا..!
حسب المعلم غمة وكآبة
مرآى (الدفاتر) بكرة وأصيلا….!!
والله ولي التوفيق.
Muhusika: duaatsalaftz
Chanzo: www.duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 15/11/2016