Hukmu ya kuvaa hereni kwa mwanamke


Swali:

Assalamu aleykum warahmatullah Wabarakaatuh
Ni ipi hukumu ya mwanamke kutoboa masikio na kuvaa heren na mfano wa hilo

Jibu

وعليكم السلام ورحمة الله وبركاته

الحمد لله رب العالمين والصلاة والسلام على رسول الله صلى الله عليه وسلم

Ndugu muulizaji:

Hakika hakuna katazo lolote la mwanamke kuvaa hereni masikioni kwani ndani yake kunapatikana pambo.

Tumtazame sheikh Ibnu Uthaymiin Allah Amrahamu wakati anajibu swali kama Hilo :-

سُئل الشيخ محمد الصالح العثيمين – رحمه الله

Aliulizwa Shaykh Muhammad Swaalih Al-‘Uthaymiin (Allaah amrehem):

عن حكم ثقب أذن البنت أو أنفها من أجل الزينة ؟

Kuhusu hukumu ya kutoboa sikio la binti au pua yake (kuweka kishaufu) kwa dhumuni la pambo.

فأجاب
Akajibu:

الصحيح : أن ثقب الأذن لا بأس به ؛ لأن هذا من المقاصد التي يتوصل بها إلى التحلي المباح

Usahihi ni kwamba kutoboa sikio ni jambo lisilo na ubaya kwasababu jambo hili linapelekea kupatikana kwa pambo mubaha.

وقد ثبت أن نساء الصحابة كان لهن أخراص يلبسنها في آذانهن

Na kwa hakika imethibiti kwamba wanawake wa kiswahaba walikuwa na vipuli wavivaavyo masikioni mwao.

وهذا التعذيب تعذيب بسيط ، وإذا ثقب في حال الصغر صار برؤه سريعاً

Na adhabu hii (ya kutoboa) ni adhabu yakuvumilika, na akitobolewa kipindi cha utoto hupona kwa mara moja.

وأما ثقب الأنف : فإنني لا أذكر فيه لأهل العلم كلاماً

Ama suala la kutoboa pua mimi sikumbuki maneno ya Wanazuoni kuhusu jambo hilo.

ولكنه فيه مُثلة وتشويه للخلقة فيما نرى ، ولعل غيرنا لا يرى ذلك

Lakini tunavyoona ni kuwa jambo hilo ni sawa na muthlah na kuharibu umbile, na huenda wengine nao wakaona kinyume chake (katika hili).

فإذا كانت المرأة في بلد يعد تحلية الأنف فيها زينة وتجملاً فلا بأس بثقب الأنف لتعليق الحلية عليه

Hivyo, akiwa mwanamke yupo kwenye mazingira ya mji ambao wanaonelea kutoboa pua ni urembo na nakshi basi hakuna ubaya (kwake) kutoboa na kuweka urembo na nakshi.

مجموع فتاوى ابن عثيمين ” ( 11 / السؤال رقم 69 )

Mhusika: Sheikh Ibnu Uthaymiin Allah Amrahamu
Mfasiri: duaatsalaftz.net
Kiunganishi: https://youtu.be/jsAJTYWv_6c
Imehaririwa: 13’J-Uwlaa/1439H