Hukmu ya maji yanayomtoka mtu katika Jimai


Swali :
Assalamu Aleykum warahmatullah
Naomba kujulishwa hukmu ya Madii na Madhii pindi yanapomtoka mtu na itampasa mtu huyo kukoga??
Jibu :

وعليكم السلام ورحمة الله وبركاته

الحمد لله رب العالمين والصلاة والسلام على رسول الله صلى الله عليه وسلم

Ndugu muulizaji:

Swali hili uliloliuliza alishaulizwa Sheikh Ibn Uthaymiin Allah Amrahamu na akalijibu swali Hilo kwa mapana zaidi.

Hivyo tutakacho kifanya sisi ni kunukuu swali na jawabu lake ambalo Sheikh Allah Amrahamu kalitolea ufafanuzi juu yake.

السؤال

إن الله لا يستحي من الحق
وسؤالي
ما يخرج من الإنسان حال
مداعبة أهله دون جماع ، ما هو؟

SWALI :
​Hakika ya ALLAH haoni haya juu ya Haqqi,​
​Swali langu : Ni kitu gani kinachomtoka mtu wakati akimchezea mkewe bila ya kufanya nae JIMAI…?​

جواب فضيلة الشيخ

الذي يخرج من الإنسان أربعة أنواع

​البول​، و ​الودي و المذي والمني​

Akajibu Sheikh Allah Amrahamu

Maji yanayomtoka mtu yapo ya aina nne :​
  1. ​MKOJO,

  2. WADII,

  3. MADHII na

  4. MANII.

 

فأما ​البول والودي​

 KUHUSU MKOJO NA WADII

فحكمهما واحد، يجب تطهير العضو منهما؛ لأن الودي ماء أبيض يكون عند
انتهاء البول هو عبارة عن بول
فله حكمه

Hukmu yao ni moja tu (nayo) inawajibika kukitoharisha kiungo , kwa kuwa
WADII​: ni maji meupee yanakuwa (yanatoka) unapoisha mkojo.
Hivyo ni mkojo .Basi una hukmu yake ( ya mkojo)

وأما ​المذي​

KUHUSU MADHII

فهو الذي يخرج بسبب الشهوة، لكنه يخرج من غير شعور به وعند برودة الشهوة، أي: أنه إذا بردت شهوة الإنسان وجد هذا البلل دون أن يشعر به

​Haya hutoka kwa sababu ya matamanio, lakini yanatoka bila ya yeye kujua na kwa wakati wa baridi ( pia hutokwa mtu na madhii ), Kwa maana matamanio yanapojiwa ( kupatwa ) na baridi, (basi) hutokwa na matone hayo ( madhii ) bila ya kuhisi chochote.​

وهذا يوجب غسل الذكر والأنثيين؛ كما أمر بذلك النبي صلى الله عليه وسلم علي بن أبي طالب، ويوجب الوضوء أيضاً، وما أصاب الثوب منه فإنه ينضح كما ينضح بول الغلام الصغير

Na hili linawajibisha kuosha tupu kiume na kike ,
Kama alivyomuamuru mtume (صلى الله عليه وسلم) Ally​ ​Bin Abii Twalib,
na inawajibisha udhu pia , na kile kilochoingia nguoni basi hicho hurashiwa rashiwa kama unavyo rashiwa rashiwa mkojo wa mtoto mdogo wa kiume,

أي

Kwa maana :-

أنه يصب عليه الماء حتى يعمه​، وبذلك يكون طاهراً

PATAMIMINWA JUU YAKE ( nguo ) MAJI MPAKA YAENEE​.
Na kwa hilo huwa ni Tohara.​

وأما ​المني​

KUHUSU MANII

فإنه ماء غليظ يخرج عند اشتداد الشهوة ويحس به الإنسان، وهذا طاهر ولكنه يوجب الغسل

​Kwa hakika hayo manii maji mazito yanatoka wakati wa kuzid matamanio na​ ​hupata hisia​ ​mwanadamu​ ​(hujisikia)​
​Na haya ( manii ) ni Twahara lakini inamuwajibikia kukoga ( ambaye ametokwa na maji hayo )

وعلى هذا فما يحدث من بعض الناس عند مداعبة زوجته من الرطوبة، إذا أحس أنه ​مني​
وهو ما يخرج ​بشهوة وبقوة وبدفق​، وجب عليه ​الغسل

​Na kwa hali hiyo kile kinachotokea kwa baadhi ya watu wakat wa kumchezea mkewe vijimaji maji ikiwa atajisikia basi ni ​MANII​​
​Nayo ni yale yatokayo KWA ​MATAMANIO, KWA NGUVU, NA KWA MCHUPO​ (mithili ya kuruka ):
Basi inamuwajibikia Kukoga

وإذا لم يكن كذلك بل أحس بالرطوبة دون أن يكون بدفق ولذة فإن هذا ​مذي​ يجب فيه غسل الذكر
والأنثيين، ونضح ما أصاب من الثياب أو من البدن

Na ikiwa haikuwa hivyo bali amehisi umaji maji bila ya

MCHUPO na LADHA(matamanio) ​ basi hii​ ni
MADHII​: inawajibika kuosha tupu ya kiume na kike kurashia rashia kikichosibu nguo au mwili.​

(mwisho wa kunukuu)

Ni matumaini yetu swali lako limejibiwa na umefaidika kwa jibu Hilo.

 

Mhusika: Sheikh Ibnu Uthaymiin Allah Amrahamu
Marejeo ya fatawa :
      http://zadgroup.net/bnothemen/upload/ftawamp3/mm_012_05.mp3
Mfasiri :duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 6’J-Uwlaa/1439