Hukumu Ya Nashidi Na Qaswida


Swali:
Ni IPI hukumu ya nashidi pia naomba kujua tofauti katika annashidi na qaswaida
Jawabu:
الحمد لله رب العالمين والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء وإمام المرسلين
وبعد.
Katika mambo ambayo tunamshukuru ALLAAH kwa uwazi wa hukumu yake katika Shari’ah yetu ya Kiislamu na fatawa za Wanazuoni wetu waliosoma wakabobea katika ‘Ulamaa wa Ahlus-Sunnah wal-jamaa (ALLAAH Awarhamu waliotangulia na kuwahifadhi waliobakia!)
Ni hili suala ambalo fitna yake imekithiri sana katika jamii ya Kiislam. Wakazeeka juu yake vijana , na kukongorojoka juu yake wazee , Ila wachache katika waliorehemewa na ALLAAH.
Ila -walillaah al-hamd- Wanazuoni wamelitolea kauli nyingi zinazokurubia kuwa ni Ijmaa kama hazijakuwa ni ijmaa.
Ntataja hapa baadhi ya kauli za baadhi yao na kukhitimisha kwa kauli nzito ya Baqiyyatus-Salaf (Al-Imaam Al-Fawzaan -ALLAAH Amhifadhi!).
(1). Al-Imaam Al-Albaaniy (Allaah Amraham!):
Yeye hakulikubali jambo hilo la anaashiid bali amelipiga vita na kutoa tamko la kutofaa kwake.
Na miongoni mwa hoja zake juu ya hilo alisema:
“Ni vyema kujenga hoja juu ya hilo kwa mambo mawili:
1. Kwamba hizi anaashiid hazikuwa katika uongofu wa Wema wetu waliotutangulia (Radhi za ALLAAH ziwe juu yao!).
2. Hali halisi inayoshuhudiwa na kujulikana ni ya khatari pia.
Na hilo ni kwasababu tumeanza kuona kwa baadhi ya vijana wa Kiislam wanapumbazika kwa hizi nashidi za kidini.
Na huwa wanazighanni daima.
Jambo ambalo limepelekea wengi wao waache kujishughulisha na kisomo cha Qur’an na kumdhukuru ALLAAH na kumswalia Mtume (swalla LLAAHU ‘alayhi wasallam)…” .
“البيان المفيد عن حكم التمثيل والأناشيد”.
(2) Al-Imaam Al-‘Uthaymiin (ALLAAH Amraham!):
“Anaashiid ziitwazo za Kiislamu ni Anaashiid za Kizushi zinafanana na zilizozuliwa na Masufi.
Na kwa hali hiyo iyapasa watu waachane nazo na waelekeze jitihada zao kwenye mawaidha ya Kitabu na Sunnah.
Ama ikiwa ni tungo ambazo zitatumika kwenye vita kusaidia kupandisha mori katika Jihadi ni jambo zuri”.
(3) Al-‘Allaamah Al-Fawzaan (ALLAAH Amhifadhi!):
“Na miongoni mwa yanayohitaji uzinduzi juu yake ni yale mambo yaliyoenea kwa wengi miongoni mwa vijana wa Dini kuhusu kanda ambazo zina sauti za watu waimbao kwa pamoja
Wanaziita kanda za anaashiid za Kiislamu na kwa uhakika ni miongoni mwa nyimbo tu.
Na huenda zikawa na sauti za kufitini (kabisa!).
Na huuzwa kwenye maduka ya studio pamoja na kanda za Qur’aan na mihadhara ya Kidini.
Na kuziita hizi nashidi kuwa ni nashiid Islaamiyyah ni jina la kimakosa (kabisa!). Kwasababu Uislamu haujatuwekea anaashiid, bali umetuwekea Dhikrillaah na Kisomo cha Qur’aaan na Ilmu yenye manufaa.
Ama anaashiid (ziitwazo) Islaamiyyah, hizo ni katika Dini za Masufi wazushi. Ambao wameijaalia Dini yao kuwa ni mambo ya kipuuzi na mchezo.
Na kuzifanya anaashiid kuwa ni sehemu ya Dini , ni /kujishabihisha na WAKRISTO….”
“AL-KHUTWAB AL-MIMBARIYYAH 3/-184-185”
Ama qaswiidah:
Ni mkusanyiko wa beti za kishairi ambazo zimeafikiana kwa wizani na vina.
Na tofauti ambayo ipo ni kuwa qaswidah inaweza kusomwa na mtu mmoja tu kwa lengo la kufikisha ujumbe fulani bila ya kujikalifisha kuiremba na kuipamba na kujitutumua.
Ama anaashiid ni mkusanyiko wa sauti za watu wanaozipamba sauti zao na kuziremba wakiwa na naghma huku wakiimba anaashiid zao.
Muhusika: duaatsalaftz
Chanzo: www.duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 15/11/2016