Makala

Ukombozi Wa (Allāh) Mneemeshaji Katika Kumjibu Mshia Muovu – 04

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 
Majibu Yetu:

Hii  nayo ni talbisi na udanganyifu mwingine wa kuendelea kujichomeka katika Uislamu.

Kuonesha kuwa Waislamu shia (!!) Wanalaumiwa na Waislamu wenzao kwa sababu ya matendo yao ambayo yanatofautiana na madhehebu nyingine, mpaka wakawadhania kuwa huenda hawafuati Qur'an na Sunnah.


Kuhusu shia kuwa si Waislamu hilo tumeshalibainisha katika makala yetu yapili, na kutaja baadhi ya kauli za Wanazuoni kama vile Imam Mālik (Allāh amrahamu), na  kuungwa kwake  mkono na Imam Al-Qurtubiy (Allāh amrahamu), na kauli za Wanazuoni wengine tulizoziacha ni nyingi mno, kwa sababu lengo ni kuwajulisha tu Waislamu ambao wanapata utata juu ya ukafiri wa hawa jamaa.

Japo si vibaya nikawataja na  wengine ambao wamewakufurisha shia Ithnay-Ashariyyah, ili mfahamu kuwa ukafiri wao si wajana wala juzi kwani hawa tutakaowaorodhesha wapo wa karne ya 2,3,4,5 mpaka ya 8, hii tuliopo ni karne ya 15 Hijriyyah :

1.Imam Ahmad bin Hanbal
Rejea: "Al-Sunnah" ya Khallāl (2/557-558).

2. Al-Bukhāriy
Rejea: "Khalqu Af-'Aalil-'Ibād" Uk (125).

3. Abū Zur-'Atir-Rāziy
Rejea: "Sharhus-Sunna" Uk (109).

4. Ahmad bin Yunus Al-Tamiimiy Al-Kūfiy
Rejea: "Al-Swārimul-Masluul" Uk (570).

5. 'Abdul-Qāhir bin Twāhir Al-Baghdādiy Al-Shāfi'iyy
Rejea: "Al-Farq Baynal-Firaq" Uk (357).

6. Ibn Hazm Al-Dhwāhiriy
Rejea: "Al-milal Wan-Nihal" (2/213).


7. Abul-Mudhaffar bin Twāhir Al-Shāfi'iyy
Rejea: "At-Tabswiir Fiyd-Diin" Uk (24-25).


8. Abū Hāmid Al-Ghazāliy Al-Shāfi'iyy
Rejea: "Al-Mustaswfā" (1/110).


9. Abul-Mudhaffar Al-Sam'āniy Al-Shāfi'iyy (Mufty wa Khurāsan)
Rejea: "Al-Ansāb" (6/341).


10. Shaykhul-Islām Ibn Taymiyyah Al-Harrāniy
Rejea: "Al-Swārimul-Masluul" Uk (586-587).


11. Abul-Fidaa Ismail bin Kathiir Al-Shāfi'iyy
Rejea: "Al-Bidāyah Wan-Nihāyah" (5/252).


12. Abū Hāmid Al-Maqdisiy Al-Shāfi'iyy
Rejea: "Risālatun-Fiyr-Radd 'Alar-Rāfidhah" Uk (200).

13. Abul-Mahāsin Al-Wāsitwiy Al-Shāfi'iyy
Rejea: "Al-Munādhwarah" (Makhtuut).


14. Sheikh Muhammad bin Sheikh Ayoub Al-Kamādhiy aliyekuwa Mudiir na Sheikh mkuu wa Madrasat Al-Shamsiyyah (TAMTA) TANGA.

Allāh awarehemu wote!

Huyu wa mwisho ametaja kwenye risala yake ya kiswahili kuwa miongoni mwa yanayomtoa mtu katika Uislamu ni kuwatukana wake wa Mtume Muhammad (swalla Llāhu alayhi wasallam), na shia wanayafanya hayo.

Na ushahidi juu hilo ni huu hapa:

Amesema Al-Majlisiy:

"Hakika Al-'Ayyāshiy amepokea kwa sanad inayozingatiwa katoka kwa Al-Swādiq (ع) kwamba Aisha na Hafsah laana ya Allāh iwe juu yao na juu ya baba zao, ndio waliomuua Mtume wa Allāh kwa sumu waliomtilia."

Rejea: "Hayātul-Quluub" cha Al-Majlisy (2/700).Ndugu msomaji! Allāh akulinde na balaa hili la ushia! Hivi baada ya yote hayo, kuna atakayethubutu kusema kuwa hawa Masheikh tuliowataja hapo juu walikuwa na ujuzi mdogo wa Uislamu?  Au kwamba wameathiriwa na fitna za maadui?


Ama kujishuku kwenu enyi shia kwamba Waislamu wanakuoneni kuwa hamufuati Kitabu na Sunnah!!

Tunasema:  Hilo si la kweli, kwamba Waislamu tuna dhana au tunakushukuni bali tuna yakini isiyo na mashaka kuwa nyinyi hamfuati kitabu wala Sunnah kabisa.

Nyinyi ni sawa na mayahudi waliomuinua 'Uzayr na  kumkataa Mtume Muhammadﷺ na nyinyi mmemuinua Aliyy juu ya Rasuulﷺ,  bali ni sawa na manaswara wanaoipinga hii Qur'an na kuiinua Injili, na nyinyi mnaikataa Qur'an yetu na kuitia dosari ma mapungufu mnakiamini kitabu kilichopo mapangoni huko kusikojulikana!!

Sasa kusema kuwa mnaonekana kama vile hamfuati Kitabu na Sunnah,  shaka hiyo ipo kwenu, lakini Waislamu alhamdulillah  mambo kwao yameshang'aa kwa waliokuwa wengi na wameshafahamu ilivyo itikadi yenu juu ya Qur'an.

Na kama mtaisoma Qur'an  yetu bado hatuna imani na nyinyi ambao ni watu wa "taqiyyah" kwani mtakuwa mnatuzuga tu na kutudhihaki!!

إِنَّ الْمُنَافِقِينَ يُخَادِعُونَ اللَّهَ وَهُوَ خَادِعُهُمْ" النساء (١٤٢).

Na pia nyinyi ni  watu wa tahriif mnaofasiri ayah kwa tafsiri za Baatwiniyyah zinazoendana na matashi yenu, neno  (بَقَرَة) "Baqarah) lililokuja  katika Qur'an lenye maana ya Ng'ombe, nyinyi mnalitafsiri kuwa maana yake ni 'Aishah!

Hivyo maana ya ayah kwenu itakuwa pale Musa ('alayhis-salaam) alipowaambia watu wake:"إِنَّ اللَّهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تَذْبَحُوا بَقَرَةً ۖ "

"Hakika Allāh anakuamrisheni mumchinje Ng'ombe"

Al-Baqarah (67).


Maana yake achinjwe mama 'Aisha!! mageni haya twayasikia toka kwenu shia hebu wapumzisheni Waislamu!

Swali: Je, 'Āishah alikuwepo zama za  Nabii Musa bin 'Imraan? Ili achinjwe na wana wa Israel??

Na tunajaribu kupekuwa katia kamusi tulizonazo za lugha ya kiarabu hatuoni kuwa katika maana ya neno  بقرة kwa mujibu wa matumizi ya lugha ya kiarabu katika maana zake ni Aisha!!


Amekukoseeni nini 'Aisha wa watu??

Au mmemfanya ni daraja tu lakini kusudio lenu ni Mtume wa Allāhﷺ??

Ndugu msomaji! Allāh akuafikishe katika haki! ukitaka kujua mtazamo wao juu ya Kitabu chetu hebu soma haya maneno yaliyoandikwa vitabuni mwao na Maimamu wao wakubwa:

Amesema Ni'matullāh Al-Jazāiriyy:

"Wamepokea khabari nyingi Masheikh zetu katika vitabu vya itikadi na hadithi na vinginevyo, kwamba (hii) Qur'an imepatwa na ukengeushwaji, mapungufu na baadhi ya ziada."

Akiwa ana maana ya  kuwa Qur'an  yetu haipo salama, kwani imetiwa mikono kwa kupunguzwa yaliyomo na kuzidishwa yasiyokuwemo.


Na bila shaka kuitakidi jambo hili dhidi ya Qur'an  hii ni ukafiri.

Sasa wao wana Qur'an  gani ambayo wanaifanyia kazi ikiwa hii yetu kwa mujibu wa itikadi yao ipo katika hali hii ya kimakosa?
 

Jawabu ni kwamba Qur'an  yao ipo Sirdaab (mapangoni), kwa Imam wao wa mwisho Al-Muntazar anayesubiriwa kutoka kutoka mafichoni. Na hili wanalithibitisha maimamu wao.


Amesema Abul-Hasan Al-'Aamiliy:

"Elewa ya kwamba ile haki ambayo haina ukwepeshaji kwa mujibu wa habari zilizopokelewa kwa wingi, ni kwamba hii Qur'an  ambayo ipo mikononi mwetu, imekumbwa na mabadiliko makubwa, baada ya kufariki kwa Mtume wa Allāh (swalla Llāhu  alayhi wasallam), na wale walioikusanya baada yake wamezichomoa ayah nyingi sana, na kwamba Qur'an yenyewe (hasa)  iliyohifadhiwa kwa mujibu wa alivyoiteremsha Allāh Mtukufu ni ile aliyoikusanya 'Aliyy, akaihifadhi mpaka ikamfikia mwanawe Al-Hasan, na ikaendelea kuwa mikononi mwao mpaka ikaishilia kwa  Al-Qāim (Imam wa 12 asubiriwaye), yuko nayo mpaka leo hii (huko mapangoni)".


Kwa maana, hii Qur'an  yetu iliyokusanywa na Abūbakr kwa ushauri toka kwa Umar (Allāh awaridhie), kisha kwa mara ya pili ikajumuishwa na 'Uthmān bin 'Affān katika Msahafu mmoja kwa lahaja moja, ambayo Waislamu wanaitakidi kuwa yaliyomo ndani yake ni maneno ya Allāh hakika, ameshuka nayo mbora wa Malaika, Jibriil ('alayhis-salaam), juu ya moyo wa mbora wa Mitume, Muhammad (swalla Llāhu  alayhi  wasallam), katika usiku uliokuwa bora zaidi, usiku wa Laylatul-Qadr, katika mwezi bora kabisa, mwezi wa Ramadhani. Wanaamini pia,  Qur'an  hii haiingiliwi na batili si mbele yake wala nyuma yake, na wanaamini kuwa  Allāh ndiye mwenyekuilinda kutokana na kuzidishwa au kupunguzwa.

Na asiyeliamini hili huyo ni kafiri kwa kuipinga Qur'an.

Our'an yetu hii si lolote si chochote mbele ya shia.

Sasa wanapotwambia shia kuwa wanafuata Qur'an  na Sunnah, wanapaswa pia watuambie ni Qur'an  ile ya pangoni (sirdaab) ambayo bado wanaingojea??, au ni hii iliyokusanywa na Abūbakr Al-Swiddiiq??  Ni hii aliyoijumuisha na kuikusanya kwa  mara yapili Uthmān bin 'Affān? Wawili hawa  ambao  kwa mujibu wa shia ni makafiri????

Na wanapotuambia kuwa wanafuata Sunnah, ni zipi hizo? Ni zile za Mtukufu  Mtume Muhammad (swalla Llāhu alayhi wasallam)? aliyesema:

"Ningelikuwa na uwezo wa kumfanya (kiumbe) kuwa ni Khalil, basi ningemchagua Abūbakr kuwa ni Khalil wangu."

Bukhari (467), na Ahmad (1/270).

Ni Sunnah iliyosema:

Alikuja 'Amru bin Al-'Aasw (Allāh amridhie), kwa Mtume (swalla Llāhu alayhi wasallam) akamuuliza:

Ni nani katika watu anapendeza zaidi kwako?

Akasema:

"Ni 'Āisha."

Nikamwambia: Katika wanaume.

Akasema:

"Ni baba yake."

Nikamuuliza kisha nani?


Akasema:

"Kisha 'Umar bin Al-Khattwāb."??

Bukhari (3662), na Muslim (2384).

Au ile  inayosema:

" Abūbakr ni wa Peponi, 'Umar ni wa Peponi, 'Uthmān ni wa Peponi...."???

Sahihi: Tirmidhiy (3747), Ahmad (1/193).

Au ni ile ya kumwambia 'Umar:

"Katu! shetani hawezi kukutana na wewe njiani ila atabadili njia na kupita njia isiyokuwa yako."

Muslim (4537), Ibn Hibbān (15/316).

Na amesema mkweli Mtume wa Allāhﷺ, shetani wa kijini anamwogopa 'Umar (Radhiyallāhu 'anhu). Japo pia wanaonekana shetani watu wanauogopa mlango katika Msikiti wa Mtumeﷺ kule Madinah uliopewa jina la 'Umar -(Baab 'Umar)- mashetani watu wanaogopa kuupita mlango huo.

فرحمة الله عليك يا أبا حفص-عمر-!!
حبك دينٌ وإيمانٌ وإحسانٌ، وبغضك كفرٌ ونفاقٌ وطغيانٌ.
 

Au ni Sunnah za Masheikh wenu akina Ni'matullāh Al-Jazaairy aliyetaja shehena ya matusi kwenye kitabu chake alichokiita "Al-An-waar Al-Nu'māniyyah"?  Matusi ya nguoni kwa Makhalifa hawa waongofu???

Ni Sunnah zipi katika hizo mnazozifuata nyinyi????

 

 

Mhusika: Al-Akh Abuu Ayman Al-Shiraaziy

Mkusanyaji: http://duaatsalaftz.net/

Nasaha

©2020 uaat Salaf Tanzania - . All Rights Reserved. Designed By Wajanjatech.Com

Search