Makala

Ukombozi Wa (Allāh) Mneemeshaji Katika Kumjibu Mshia Muovu – 05

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 

Majibu Yetu:

Muislamu Msunniy anakiri kuwa katika zama zetu hizi yamejaa makundi mengi na mapote ambayo yanakwenda kinyume na uongofu wa Mtume Muhammadﷺ na ufahamu wa Maswahaba zake (Allāh awaridhie), na  kwa bahati mbaya mapote yote hayo yanajinasibu na  Uislamu.

Na Muislamu Msunniy anaitakidi kuwa hakuna katika Uislamu Jamaa inayokubalika zaidi ya Jamaa ya Ahlus-Sunnah, na hakuna njia itakayoridhiwa isipokuwa njia moja tu ya Mtukufu Mtume Muhammadﷺ na Swahaba zake wateule (Allāh awaridhie).

Ambao amewasifia pale alipotaja makundi yanayokwenda kinyume na haki akasema:

((... وتفترق أمتي على ثلاث وسبعين ملة كلهم في النار إلا واحدة، قالوا: ومن هي يا رسول الله؟ قال: ما أنا عليه وأصحابي))

"..Na utatofautiana Ummah wangu juu ya makundi sabini na matatu, yote yataingia motoni ila kundi moja tu. Akaulizwa: Ni lipi hilo Ewe Mtume wa Allāh! Akasema: Ni lile litakaloshikamana na ambayo nipo nayo (leo hii) na Swahaba zangu."

Ameipokea: Tirmidhiy (2641) kutoka kwa Ibn 'Amr, na Abū Daud, kutoka kwa Mu'aawiyah, na Ibn Mājah kutoka kwa Anas bin Mālik na 'Awf bin Mālik.

Itakuwa ajabu kwa Waislamu Wasunniy kuyaacha ya Mtume na Swahaba zake, kisha wayapokee ya mashia watoto wa zao la mut'ah na  watusi wa Maswahaba!!

Hivyo tunaamini kuwa hatuna Jamaa isipokuwa ni ile moja tu (Jamaa mama), ambayo ni Jamaa ya Ahlus-Sunnah, na hatuna njia nyingi, zaidi ya  njia moja tu ambayo ni  ya Mtume Muhammadﷺ na Maswahaba zake, na hatuna kiongozi atuongozaye ila ni  Mtume Muhammadﷺ, hatuna mwengine tunayemkubali kutuongoza katika Dini zaidi yakeﷺ.


Amesema Allāh Mtukufu:

"اتَّبِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۗ " الأعراف (٣).

"Fuateni mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu, wala  msifuate wengine (katika wasimamizi) badala yake."

Al-A'rāf (03).


Na bila shaka tulichoteremshiwa kutoka kwa Allāh Mola wetu ni Kitabu na Sunnah.

Na bila shaka hao tuliokatazwa tusiwafuate ni wale wanaoamrisha ushirikina na kuabudia mizimu na masanamu, kwani hao ni wapotoshaji si waelekezaji.

Na hayo ndiyo aliyoyasema Imam Twabariy katika hii ayah.

Na sifa hizo zinawaingia pia shia. Kwamba ni watu wa shirki wenye kuwaomba viumbe badala ya Allāh -(labbayk ya Husein!!)- na ni watu wazushi na wapotevu, kila balaa lipo kwao.


أهل البدع والزيف والمنكر
والشرك بأشكاله وبأنواعه.


 Na alhamdulillah, Ahlus-Sunnah  wametosheka na mafunzo ya Dini yao kutoka kwa Mtume waoﷺ kupitia kwa Maswahaba Wateule Waaminiwa, kiasi kwamba hawahitajii kutoka kwa yeyote chochote, kwa kuamini kwao kuwa Dini ilishakamilika. Imekamilika katika mfumo mzima wa Ibada, imekamilika katika mfumo wa Miamala, iko kamili katika upande wa Itikadi, Iko kamili katika nyanja na  taratibu za linganizi zake, imekamilika katika suluki akhlalqi na tabia njema, kwa namna ambayo hawasubirii Waislamu maelekezo ya Ibada kutoka kwa wamajusi wa Iran wala waabudu moto wa peshia.

Amesema Mtumeﷺ:

"قد تركتكم على البيضاء ليلها كنهارها لا يزيغ عنها بعدي إلا هالك، من يعش منكم فسيرى اختلافا كثيرا، فعليكم بما عرفتم من سنتي وسنة الخلفاء الراشدين المهديين عضوا عليها بالنواجذ".

"Hakika nimekuacheni katika uwanja mweupe usiku wake sawa na mchana wake hapotei baada yangu ila mwenye kuangamia. Atakayeishi (kitambo kirefu) miongoni mwenu atakuja kuona tofauti nyingi. Basi ni juu yenu kushikamana na mwenendo wangu muujuao na mwenendo wa Makhalifa wangu Waongofu walioongozwa, ushikilieni (mwenendo huo) kwa meno ya magego."

Ameipokea Ibn Mājah kutoka kwa Al-'Irbādh bin Sāriyah.

Atakuwa na kichaa cha bimtoo kumpa maiti shikamoo Msunniy ambaye Mtume wake anamtaka ashikamane na  mwenendo wake na mwenendo wa Swahaba zake, alafu yeye (Msunniy) ashikamane na mwenendo wa Khomeni Imam wa upotevu mkashifuji wa Dini ya Kiislamu na Nabii wake.

Sasa Waislamu Sunniy hawana hitajio la kufunzwa matendo ya shia kwa sababu hawajapungukiwa wala hawana mashaka juu ya Dini yao na mafunzo yake walillāh alhamdu.

Uthibitisho juu ya hilo, hamuwasikii Sunniy hata siku moja katika adhana zao wakisema:

"Ash-hadu anna 'Aliyyan Waliyyullaaaaah!!."


Wala wakisema:

"Hayya 'alaa khayril-'amal."

Kwa kuwa yale mapokezi ya sifa ya adhana waliyopokea kutoka kwa Maswahaba kama vile 'Umar bin Al-Khattwāb na 'Abdullāh bin Zayd (Allāh awaridhie) yakakubaliwa na Mtume Muhammadﷺ yamewatosha.


Halafu kusema kwamba matendo hayo yana asili katika dini hamuoni kuwa ni talbiis na udanganyifu huo? Au mwaona raha pale mnapoambiwa  shia waongo?

Yana asili katika Dini!  Ni Dini ipi moja wapo?

Allāh amrehemu Imam wetu Shaafi'iyy, pale aliposema:

"Sijawahi kumwona yeyote katika watu wazushi muongo mkubwa katika madai, muongo mkubwa katika kutoa ushuhuda kama vile shia."

Rejea: "Al-Ibānatul-Kubraa" (2/545).


Sisi Waislamu tumetofautiana na shia katika kila kitu labda tu maumbile tuliyoumbiwa na Allāh Muweza, kwamba  Sunniy ana pua ya kunusia na shia naye ana pua. lakini kwenye Dini tupo kinyume kabisa, hatukutani nao si kwa mbali wala kwa karibu.

الحمد لله الذي عافانا مما ابتلاكم به!!


-Tumetofautiana katika adhana.

-Udhu wao si sawa na Udhu wetu.

-Iqama yao si  Iqama yetu.

-Nyakati za swala zao si nyakati za swala zetu.

-Jinsi wanavyoswali wao si sawa na  kuswali kwetu.

-Itikadi yao juu ya Qur'an  si Itikadi yetu.

-Itikadi yao juu Mtume Muhammadﷺ, si Itikadi yetu.

-Itikadi yao juu Maswahaba (Allāh awaridhie), si Itikadi yetu.

-Itikadi yao juu ya wake wa Mtumeﷺ, si Itikadi yetu.

-Itikadi yao juu ya taraweh si Itikadi yetu.

-Itikadi yao juu ya muda wa kufturu na kufungua si Itikadi yetu.

-Itikadi yao juu ya kuwapongeza Manaswara kwa Idd zao  na Xmas zao si Itikadi yetu.

-Kuruhusu kwao kuwaingilia wanawake kwa nyuma si ruhusa kwetu.


ضدان لا يجتمعان ولن يتلاقَيا
             حتى تشيب مفارق الغربان.Na kusema kuwa matendo ya shia yanafaa kufanywa na Waislamu wote.


Yaani mna talbis na udanganyifu mbaya sana -قاتلكم الله- kana kwamba mmewahi kusikia fununu za malalamiko kutoka kwa Waislamu kuwa sasa mbona  wenzetu shia hawataki sisi kufanya Ibada zao!!

Kisha baada ya hapo jopo la mabwana wakubwa wakakaa kimashauriano na kutoa neno la pamoja kuwa waruhusuni tu Waislamu Sunniy na wao wapate kutononeka na Ibada zetu za Karbalaa!!  

Hiyo  ni Lugha ya kutaka kuwatumbukiza Sunniy katika dimbwi chafu la ushia.

Lakini himdi ni za Allāh, kisha shukrani kwa Masheikh zetu waliotuzibua masikio na kututoa vibanzi vya macho, kwa kutubainishia juu ya ukafiri na uovu wa shia kutoka katika vitabu vyao tegemewa.

 

 

Mhusika: Al-Akh Abuu Ayman Al-Shiraaziy

Mkusanyaji: http://duaatsalaftz.net/

Nasaha

©2020 uaat Salaf Tanzania - . All Rights Reserved. Designed By Wajanjatech.Com

Search