Makala

Ukombozi Wa (Allāh) Mneemeshaji Katika Kumjibu Mshia Muovu – 06

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 
Majibu Yetu:

Amesema Allāh Mtukufu:

"لِيَحْمِلُوا أَوْزَارَهُمْ كَامِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۙ وَمِنْ أَوْزَارِ الَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ" النحل (٢٥).

"(Wanapoteza watu hivi) ili wabebe mizigo (ya madhambi) yao kamili Siku ya Kiyama na (pia) sehemu ya mizigo ya wale wanaowapoteza bila ya kuwa na ilimu (hao wanaowapoteza). Sikilizeni! Ni mibaya mno hiyo (mizigo) wanayoibeba."

An-Nahl (25) Al-Farsy.


Na amesema Mola Mtukufu:

"وَلَيَحْمِلُنَّ أَثْقَالَهُمْ وَأَثْقَالًا مَّعَ أَثْقَالِهِمْ ۖ وَلَيُسْأَلُنَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَمَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ" العنكبوت (١٣).

"Na hakika wataibeba mizigo yao, na mizigo mingine pamoja na mizigo yao (nayo ni mizigo ya dhambi za kuwapoteza wenziwao, na hao wenyekupotezwa watachukua mizigo ya kukubali kufanya makosa). Na kwa yakini wataulizwa Siku ya Kiyama juu ya yale waliyokuwa wakiyazua."

Al-'Ankabūt (13), Al-Farsy.

Amesema Imam Mujāhid bin Jabr (Allāh amrahamu):

"يحملون أثقالهم: ذنوبهم وذنوب من أطاعهم، ولا يخفف عمن أطاعهم من العذاب شيئا".


"Watabeba mizigo yao; kwa maana dhambi zao na dhambi za wale waliowatii. Na wala waliotii hawatopunguziwa chochote katika adhabu."

Rejea: Al-Jalālayn.


Nasaha zetu kwa huyo mnayemshukuru kwa chumo baya la mkono wake (mwana wa Okhaya) ni airudie nafsi yake, na atubu kwa Allāh na kurudi katika Dini ya ya Kiislamu, Dini ya  haki, kwani Allāh anapokea toba kutoka kwa waja wake muda wa kuwa hawajafikwa na umauti wala kufika wakati wa kutokukubaliwa kwa toba zao.  

Na aihurumie nafsi yake juu ya mchango mkubwa anaoutoa yeye na mithili yake katika kuwaritadisha Waislamu Ahlus-Sunnah Waljamā'ah wasiojua kubaini juu ya hila za shia na udanganyifu wao kwa kuvifanyia tarjamah vitabu vyao vya upotevu kwa jamii ya Waislamu wasomao kiswahili.

Wejuwe ya kwamba, makemeo juu ya hili ni makali sana kutoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad ﷺ, kwa watu waharibifu mithili yao, wenye kuacha athari mbaya za wino wao mweusi na vitabu vyao vyeusi.

Amesema Mtumeﷺ:

((من دعا إلى ضلالة كان عليه من الإثم مثل آثام من تبعه لا ينقص ذلك من آثارهم شيئا)).

"Yeyote atakayelingania kunako upotevu, atapata madhambi mithili ya madhambi ya watakaomfuata, na hilo halitowapunguzia chochote katika madhambi yao."

Muslim.

Na msababishaji wa jambo huwa sawa na mfanyaji, kwa maana wakiratadi watu Mia moja wakaingia ushiani basi dhambi za kila mmoja katika hao atazibeba mwana wa Okhaya kanakwamba yeye ndiye ameritadi  kwa idadi hizo (japo naye ni katika hao hao).

Na bila shaka ikitokea amekufa, basi itakufa tu nafsi yake, kuwa haipo tena duniani lakini hubaki athari yake itakayoendelea kuwapoteza watu mpaka siku ya Kiyama na yeye kupata fungu lake hapo kaburini alipo, mpaka pale litakapopulizwa Baragumu.


Hivyo jambo ni hatari zaidi ya tunavyodhania na kufikiria. Magari haya tunayozunguka  nayo, majumba ya kifakhari yanayo tuhifadhif, pesa tunazotononeshwa nazo vyote hivyo ni mapito na akhera ndio kwenye marejeo ya kudumu.

Akhera ni  bora na ni yenye kubakia. Bora tuwe na subira kwa uduni wa hali tuliyonayo kuliko kuiuza Dini yetu na Itikadi yetu ya Ahlus-Sunnah kwa thamani chache za kilimwengu tuzipatazo kutoka  katika mali za khumsu.

Amesema Allāh Mtukufu:

"مَا عِندَكُمْ يَنفَدُ ۖ وَمَا عِندَ اللَّهِ بَاقٍ ۗ وَلَنَجْزِيَنَّ الَّذِينَ صَبَرُوا أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ" النحل (٩٦).

"Mlivyo navyo vitakwisha na vilivyoko kwa Allāh (vya jazaa yenu) ndivyo vitakavyobakia. Na kwa yakini Sisi tutawapa waliosubiri ujira wao (mkubwa kabisa) kwa yale mazuri waliyokuwa wakiyatenda."

An-Nahl (96).

Japo tunaamini ya kwamba kutoka katika ushia baada kuonja ladha zake ni jambo lenyekuhitajia tawfiiq kutoka kwa Allāh, kwani ushia unawapambia mashia kupenda mambo ya hanasa kwa ismu ya Dini. Hivyo huwa shida kubwa sana na hasa pale unaposimamiwa na shetani wa kijinni.

Tunafahamu kuwa shia wanatumia kila njia kuwateka kimaslahi Masheikh wa kisunniy ili hata kama wasipoingia katika ushia basi ile sura ya kuonekana wapo pamoja nao wanashirikiana katika mambo yao kwao (shia) ni hatua kubwa sana.


Lakini tunafahamu kuwa wana njia nyingi sana katika kuwaritadisha  Waislamu  na kuwaingiza katika ushia wao na ukafiri.

Miongoni mwa hanasa za shia:

-kuswali kwao vipindi vitatu  kwa siku. Na katika hanasa hii wanawateka sana waajiriwa wa maofisini na wenye udhaifu wa Kiiymani.

-ndoa za mikataba (mut'ah). Kumchukua umtakaye, na kwa idadi uitakayo, hakuna shahidi wala walii mnaozeshana nyinyi wenyewe tu, yaani binti na kijana. Na katika hanasa hii wameweza kuwateka lukuki ya shabaab, na vijana wanaopenda mporomoko. Wakawachukua binti za watu kwa kile kilichoitwa kuifanyia kazi ndoa ya Mut'ah na kuwapeleka katika nyumba za wageni bila ya wazazi wao kujua, kwa sababu ndoa hii haishurutishi kumtafutia mwanamke makazi wala huduma ya aina yoyote.

- kumuingiza mtu katika ushia kuna kiwango maalumu cha baqshishi atakachopewa yule aliyefanya jitihada hiyo, hivyo anapewa kama ahsante kutoka kwa wakuu.

-kupeleka watu masomoni nje, ima iwe Nairobi, Lebanon, Iraq au Iran na kwengineko. Na hili wanawanasa sana wale ambao hawajawahi kuwaza kuwa ipo siku atabahatika na yeye kupanda ndege, hivyo akihakikishiwa ya kuwa atapanda ndege na kutolewa vumbi la macho basi hakuna kinachobaki zaidi ya yeye kuuza Uislamu wake na  kuingia ushiani kwa ulimbukeni wa kukweya pipa kama wanavyosema.

-Kuruhusu kwao juu ya kufaa kuwalawiti wake zao. Jambo ambalo shetani wa kijinni wanawapambia tabia hiyo chafu na dhambi kuu katika madhambi makuu mashetani wa kibinaadamu, leo hii jambo hilo shia wanaliruhusu na kuliwekea thawabu na malipo.Hivyo ukishayadhuku hayo na mfano wake kutoka ushiani kwako ni tawfiiq kutoka kwa Allāh na wala si kwa msukumo wa Iymani, bali ni Allāh akudiriki kwa Rahma Zake.

وقد فعل (سبحانه) بأناس كانوا من أعيان الشيعة الروافض.

Na yote hayo ni sababu ya njaa iliyoendekezwa.
 
Ila wallah! Lau njaa ingelikuwa na nafasi kubwa ya kuwapoteza watu basi wangelipotea  kwanza Maswahaba wa Mtume Muhammadﷺ, kwani ilifika siku hawana chakukila zaidi ya majani ya miti mpaka wakawa wanatoa kinyesi mithili ya kinyesi cha mbuzi, huku wakiwa na majeraha  katika mafizi yao na mashavu yao kwa ndani kwa sababu ya kula majani ya miti,  hili liliwafika wao pamoja  na Mtume wao Muhammadﷺ, kama alivyolisimulia hilo Swahaba 'Utbah bin Ghaz'wān (Allāh amridhie).

Kikubwa tunakunasihini enyi mliolelewa na wazee wenu ambao ni Ahlus-Sunnah, bali baadhi yenu mliafiqishwa kukaa na kulelewa katika  majumba ya Masheikh wa Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa miaka nenda miaka rudi, kipi kimekughurini na kukuhadaeni kama si hanasa mzipatazo huko? pesa na  kubadili wanawake kwa jina la ndoa ya mut'ah??

وقديما قيل:

إذا كان الطباعُ طباعَ سوءٍ  
          فلا أدبٌ يفيد ولا أديبُ.

Kumbukeni kuwa ushia ni uyahudi, na unapowaona mayahudi wanakung'ang'ania fahamu kuwa si kwa sababu ya pendo la dhati juu yako  bali wanataka kupitia kwako wapitishe yale yao wayatakayo, wakishamaliza kukutumia wanakutupilia mbali mithili ya tambara bovu au mwanamke kahaba. na mifano ya hili huko kwenu ushiani ni mingi.

Allāh amridhie Swahaba Hudhayfah Ibn Al-Yamān! Hakika amesema kweli (radhi za Allāh ziwe juu yake), pale aliposema:

"فاعلم أن الضلالة حق الضلالة أن تعرف ما كنت تنكره، وتنكر ما كنت تعرفه، وإياك والتلون فإن دين الله واحد" (المطالب العالية)."Elewa ya  kuwa, upotevu mkubwa ni kukikubali ulichokuwa unakipinga (kabla), na kukipinga ulichokuwa unakikubali. Ole wako na kubadilikabadilika kwani Dini ya Allāh ni moja (tu)."

Na nyinyi zama ambazo shia walikuwa ni wale wahindi tu akina gabachori na pateli,mlikuwa mkiupinga  ushia na kuyaona yale yao kuwa ni kinyaa, kipindi ambacho wakitajwa Makhalifa wanne juu ya mimbari mnasema (RadhiyaLlāhu-'anhum!!), leo hii baada ya kuingia ushiani, na kujengewa  masinagogi zenu za watu weusi (Bilāl) mkatenganishwa na shia weupe akina Patel na gabachori  watajwapo Makhalifa waongofu (Allāh awaridhie) mnawalani!!


نعوذ بالله من الحَوْرِ بعد الكَوْرِ!! ومن الضّلالة والعَمى بعد الهُدى!!


Enyi shia!!

Kwa nini tunakuiteni katika uokovu na uongofu,  nanyi mnatuita kwenye Moto?

Mnatuita tumkufuru Allāh na kumshirikisha na yule Husein wa karbalaa ambaye hatumjui (kwa mujibu wa itikadi zenu), nasi tunakuiteni kwa Allāh Mwenye nguvu Mwingi wa msamaha!!

Bila shaka mnatuita kwenda kuwaabudu ambao hawana wito duniani wala Akhera, na marejeo yetu ni kwa Allāh. Na wanaopindukia mipaka (kama nyinyi) hao ndio watu wa motoni.

Mtayakumbuka haya tunayokuambieni. Na sisi tunamkabidhi mambo yetu Allāh. Hakika Allāh anawaona waja wake.

Amesema Allāh Mtukufu:

"وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّهِ الْكَذِبَ وَهُوَ يُدْعَىٰ إِلَى الْإِسْلَامِ ۚ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ" الصف (٧).


"Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule anaye mzulia Allāh  uwongo, naye anaitwa kwenye Uislamu? Na Allāh hawaongoi watu madhaalimu."

Al-Swaff (07).صدق الله العظيم.

 

Mhusika: Al-Akh Abuu Ayman Al-Shiraaziy

Mkusanyaji: http://duaatsalaftz.net/

Nasaha

©2020 uaat Salaf Tanzania - . All Rights Reserved. Designed By Wajanjatech.Com

Search