Makala

Ukombozi Wa (Allāh) Mneemeshaji Katika Kumjibu Mshia Muovu – 07

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 
Majibu Yetu:


Shia huko mlipolalia ndipo wenzenu  walipoamkia, yaani mnaleta taswira ya kuulilia umma wa Kiislamu kutokana na kule kupasuka kwake mkaonesha huzuni zenu za juu, na kwamba ni jambo linalowashughulisha kiasi kwamba mnakesha katika kulitafutua ufumbuzi wake wa kina kanakwamba na nyinyi mpo ndani ya Uislamu!

Mfano wenu ni sawa na yule mtu aliyempiga mwenzake kofi  kisha akaonekana kuwa analia yeye!!

 Hebu wapumzisheni kwanza Ahlus-Sunnah,  kwani wamechoshwa na talbiis zenu na udanganyifu wenu.


Kama ni ukoloni basi nyie shia ndio mnaoendeleza kuuelekeza umma wa Kiislamu katika  ugomvi na uadui, mnaopandikiza mbegu za kasumba na mifarakano na mkazimwagia mbolea za hasada na chuki baina ya Waislamu Ahlus-Sunnah Waljamā'ah wao kwa wao!  

Nyinyi ni sababu kuu ya mifarakano iliyopo baina ya Ahlus-Sunnah  wao kwa wao kwa sababu nyinyi ndio mnaowachomekea mambo ya kizushi katika Dini yao, na bila shaka uzushi unagawa watu.

 limetoka wapi dhehebu la tano muliitalo "Wahabiyah" kama si kampeni zenu na njama za kutaka kuwakimbiza watu wenye mashrabu mamoja ili wasikae pamoja na kunasihiana katika haki? Ambao ima watakuwa ni mahanafiy, au maalikiy, au hambaliy, au mashaafiy,   lakini nyinyi wafitini wakubwa hamkupendezwa na hali ya umoja walionao Ahlus-Sunnah Waljamā'ah  mpaka pale mlipoanzisha pekepeke na fitina kama ilivyo jadi yenu ya toka tangu, lengo lenu kuu ni kuwafarikisha Waislamu ili mpate kuwateka na kuwatala!!

Ndipo pale wanaposimama sehemu ya Waislamu Ahlus-Sunnah kuwakemea na kuwatahadharisha Waislamu wenziwao kuhusu mambo kadhaa wa kadha katika Dini nyinyi ndio vinara mnaosimama na kuvuvumkwa na kuwaambia Waislamu kuwa hao wanaokataza kujengea makaburi ni mawahabi hao msiwasikilize! Kanakwamba Imam Shaafiy wetu Allāh amrahamu hajalipinga hilo! Si ndio nyinyi wakoloni mnaoendelea kuzibaka na kuziteka akili za baadhi ya masunniy huku mkiwa mnawaghuri kwa visafleti vya michele na madumu ya mafuta? Mkawalewesha navyo hivyo mpaka wakalewa!? Na mkatumia uhodari wa kipumbavu katika kuwafikishia kusudio lenu mpaka mkafanikiwa kuugawa umma wa Kiislamu wa Ahlus-Sunnah, mpaka wakawa wanatazamana kwa ubaya wao kwa wao ilhali wote ni kitu kimoja ndugu moja!? Tangu zama zile ambazo shia walikuwa ni wahindi tu hapa nchini mpaka leo hii wameweza kuwarubuni vilivyo wakapatikana shia weusi ambao mnawaritadisha kwa husuda tu mlizonazo!

Tendo lenu hilo linasadikisha kauli ya Allāh Mtukufu:

"وَوَدُّوا لَوْ تَكْفُرُونَ" الممتحنة (٢).

"Na wanapenda muwe makafiri."

Al-Mumtahanah (02).

"وَدَّ كَثِيرٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يَرُدُّونَكُم مِّن بَعْدِ إِيمَانِكُمْ كُفَّارًا حَسَدًا مِّنْ عِندِ أَنفُسِهِم" البقرة (١٠٩).

   " Wengi miongoni mwa watu wa Kitabu wanatamani Lau wange kurudisheni nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa ajili ya uhasidi uliomo ndani ya nafsi zao."

Al- aqarah (109).


Ni husda tu, waila, wamtoaje mtu katika Dini yake ya haki na kumrubuni aje katika dini yako kwa pesa na vyakula!? Kisha  ukampa amri na makatazo, kisha akayashikilia na kujitahidi kutenda kisha atakapokufa haendi kuingia Peponi!  Kama si hasadi hii ni nini??

Na kwani kuna jengine walitakalo watu wanaowafuata Mitume wao na Manabii kikamilifu zaidi ya kupata pepo ya Mola wao na kuepushwa na moto wake? Na hili ni kwa watu wa Dini zote na mila zote, kwamba wanajitahidi kufata uongofu na kujiepusha na upotofu ili waingie peponi.

Wakawa hawa wanataka pepo (Al-Jannah), na wale wanataka uzima wa milele.

Kwa maana wanafanya yote hayo kwa lengo kubwa hilo.

Sasa kwa bahati mbaya hilo kwa shia weusi halipo.

Kwa maana pepo haitoingiwa na aliyemweusi.


Na haya si maneno yetu, bali ni hadithi yao iliyosihi katika vitabu vyao tegemewa.

Ameitaja hii hadithi sheikh wao Al-Majlisiyy katika kitabu chake:

 "Bihārul-An-waar" (Juz 96/Uk 192).

Atakuwa ana dhambi gani mtu mweusi kwa sababu ya weusi wake?

Na kama hatoingia peponi kwa nini mnapoteza khumsu (pesa) zenu kwa mtu ambaye jema lake na ovu lake ni sawa!?

Afanye afanyavyo katika wema ila pepo kwake itakuwa kama chongo ya mkwewe!

Jumla ya kauli ni kuwa wakoloni ni nyinyi, na munayo makoloni yenu katika wadhaifu wa Iymani miongoni mwetu na hili hatulipingi kwani tulishaambiwa na Mtume wetu (swalla Llāhu  'alayhi wasallam) kuwa "watu ni sawa na madini", yapo ya ghali na yapo ya kati na kati, na yapo yaliyo duni thamani, ambayo ukipewa utayatumia tu katika kufanya istijmaar au kusugulia sagamba za miguu. Na mkitaka kulijua hilo ni kile kipindi cha baadhi ya Masheikh na Du'aat wa kheri (Allāh awahifadhi) walipokuwa wakiendesha operation  yao kabambe ya kubainisha juu ya  Fadhila za Maswahaba wa Mtukufu Mtume Muhammad  (swalla Llāhu 'alayhi wasallam), na kuwazindua Waislamu juu ya uovu wa watusi wa Maswahaba (Allāh awaridhie) hapa nchini (bara na visiwani), na kwa kuwa Waislamu  ni wamoja mbali na madhehebu zao mashuhuri nne walikuwa wakipita na  kuomba nafasi katika Misikiti ya Wailsamu wenziwao (hawakuja kwenye masinagogi zenu) na wanapewa, ila Misikiti miwili ambayo ina  makolono ya shia, mmoja ni Msikiti uliopo  katika moja ya mitaa ya K/koo, na mwengine ni  magomeni, walikubaliwa Masheikh hao katika Ahlus-Sunnah, kisha ghafla kabla ya kufika siku husika ya kufanyika kwa Nad-wah hiyo wakoloni nyie (قاتلكم الله) mkawapigia makoloni yenu na kuwataka wazuie mara moja, na kweli yale makoloni yenu -(Allāh ayaongoze au ayavunje migongo yao)- yakatii amri zenu.

هم أعمى البصر والبصيرة

Sasa mnalilia wakoloni gani wengine?

Ikiwa mmeweza kubaka akili za wapumbavu wetu na wao jinsi walivyolewa wakashindwa hata  kutafakari juu ya uzito wa mada "fadhila za Maswahaba"!!  kikubwa kwa kuwa wanapata maslahi yao ya kuvimbisha matumbo yao wakatii agizo kutoka kwa mabwana wakubwa na mabwanyenye wao.

Na hana jina jengine anayeweza kuchukua badali akaacha chema akachukua kibaya zaidi ya kuwa ni mpumbavu.

Allāh amewalaumu mayahudi kwa jambo kama hilo.

 "قَالَ أَتَسْتَبْدِلُونَ الَّذِي هُوَ أَدْنَىٰ بِالَّذِي هُوَ خَيْرٌ ۚ " البقرة (٦١).

"Mnabadili kilicho duni kwa kilicho bora?."

Al-Baaarah (61).

Ila kiukweli himdi zote anastahiki Allāh Muumba wa mbingu na ardhi. Wengi wa Waislamu waliokuwa wakikudhanieni kuwa nanyi ni miongoni mwao leo wameshakueleweni kwa kiasi kikubwa, na wengi wao si tu wamewatoa vijana wao katika zile zinazoitwa madaarisi zenu (hawzah), ambazo mnawakusanya mabinti wa watu vigori kutoka mikoani na vijijini kwa kile mnachokiita mnawafunza kazi za mikono na kuwafanyia mut'ah bali wamewatoa mpaka kwenye maskuli yenu ambayo mnawaingizia ushia kwa ismu ya masomo ya Kiislamu mashuleni.

Amesema Allāh Mtukufu:

"وَمَكَرُوا مَكْرًا وَمَكَرْنَا مَكْرًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ" النمل (٥٠).


  Na wakapanga njama zao Na sisi tukazibatilisha (kwa kuwawahishia adhabu) ilhali hawajui kitu."

An-Naml (50).

Hivyo ni Sunnah ya Alla kubatilisha vitimbi vya watu waovu mithili yenu.

 pamoja na hila zenu nyingi na njama katika kuwaritadisha Waislamu Ahlus-Sunnah  lakini njama zenu na uovu wenu umefichuka kwa Waislamu na unaendelea.

Amesema kweli Allāh Mtukufu:

"مَّا كَانَ اللَّهُ لِيَذَرَ الْمُؤْمِنِينَ عَلَىٰ مَا أَنتُمْ عَلَيْهِ حَتَّىٰ يَمِيزَ الْخَبِيثَ مِنَ الطَّيِّبِ ۗ " آل عمران (١٧٩).


Haiwi kwa Allāh kuwaacha Waumini katika hali mliyo nayo mpaka apambanue wabaya na wema."

Al-'Imrān (179).

Sifa zote njema anastahiki Allāh Mtukufu mwenyekutimiza ahadi zake, leo hii Waislamu wamebainikiwa na mengi dhidi yenu enyi shia wa shetani, Allāh kawayafichua mliyoyaficha vifuani mwenu, leo hii anatokea mmoja wenu anayejiita hamza wa mayunga anaandika makala kwa lugha ya kiswahili ndani yake anathubutu kusema kuwa anayemtukana Abūbakr Al-Swiddiq Khalifa wa kwanza wa Mtukufu Mtume Muhammad (swalla Llāhu 'alayhi wasallam) anapata thawabu!!!!!!?

Na wakasikika wengine wakiwa wanamtupia tuhuma za zinaa na machafu mke wa Mtukufu Mtume Muhammad (swalla Llāhu 'alayhi wasallam) mama wa Waumini Aisha kipenzi cha Mtume na  bint wa Abūbakr Al-Swiddi (Allāh amridhie)!!

فَإِنّا لِله وإنا إليه راجعون.


اللهم عليك بهم فإنه لا يعجزونك!!Wito!!

Ni wajibu kwa kila Muislamu mwenye ghera (uchungu) na upeo wa ilmu ya Dini yake ya Kiisalmu na ndugu zake Waumini ajitahidi kuitwaharisha jamii yake ya Kiislamu kutokana na itikadi za hawa watu pamoja na athari zao, na hilo halitawezakana kikamilifu ila kwa kueneza ilimu iliyokuwa sahihi, na kufundisha Tawhiid waliyokuja nayo Mitume ('alayhimus-Salām), ili kuondosha dhima mbele ya Allāh Subhānahu wata'ālaa, Kila mmoja kwa nafasi yake.

 

Mhusika: Al-Akh Abuu Ayman Al-Shiraaziy

Mkusanyaji: http://duaatsalaftz.net/

Nasaha

©2020 uaat Salaf Tanzania - . All Rights Reserved. Designed By Wajanjatech.Com

Search