Makala

Ukombozi Wa (Allāh) Mneemeshaji Katika Kumjibu Mshia Muovu – 08

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 
Majibu Yetu:

Amesema Allāh Mtukufu:

"إِنَّمَا ٱلْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُواْ بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ" الحجرات (١٠).

 "Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Allāh ili mrehemewe."

Al-Hujurāt (10).


Na udugu huu haupo isipokuwa katika Dini.

Na hili ndilo walilolisema Jumhuri ya Wanazuoni wa Tafsiir ya Qur'an.

Amesema Ibn Kathiir Al-Shāfi'iyy (Allāh amrahamu):

"(Ay!)Maana yake: Wote ni ndugu katika Dini, kama alivyosema Mtumeﷺ: "Muislamu ni ndugu wa Muislamu, hamdhulumu wala hamsalimishi."


Na amesema Imam bin Nāsir Al-Sa'diy (Allāh amrahamu):

"Huu ni mkataba uliowekwa  na Allāh  baina ya Waumini, kwamba itakapopatikana kutoka kwa mtu yeyote katika mashariki ya ardhi na magharibi yake, Iymani ya kumwamini Allāh na Malaika wake, Vitabu vyake, Mitume wake na Siku ya mwisho, basi huyo ni ndugu wa Waumini (Waislamu), tena udugu ambao unawajibisha wampendelee wayapendayo nafsini mwao,   na wachukie kwa ajili yake wanayoyachukia nafsini mwao."

Rejea: "Taysiiril-Kariim" katika Ayah tajwa hapo juu.

Bila shaka tumevuna faida hapo kuwa udugu unaokusudiwa ni udugu wa Dini, sio udugu wa taifa, kanda, kabila, rangi  wala nasaba.

Na udugu wa Dini haupatikani bila ya kuwa pamoja katika Itikadi. Na ndio maana Imam 'Abdur-Rahmān Nāsir Al-Sa'diy Al-Hanbaliy (Allāh amrahamu), akaligusia hili katika maelezo yake alipokuwa akiifasiri Ayah hii.  Ametaja kumwamini Allāh, Malaika wake, Vitabu, Mitume na Siku ya mwisho.

Ili  tuwe na udugu na shia ni lazima tuwe pamoja katika masuala ya Ki-Iymani na Itikadi.


Swali: Je, shia wapo na sisi katika hayo?


Jawabu hili hapa tunapatiwa  na mwanazuoni wao bingwa   wa hadithi katika zama zake,  Ni'matullāh Al-Jazāiriyy (ilikuwa sawa aitwe Khasāratush-shii'ah Al-Jāhiliy):

"Hakika sisi hatujumuiki nao (yaani Masunniy) katika Mola, Nabii wala Imam. Na hilo ni kwa sababu ya kuwa wao (Sunniy) wanasema kwamba Mola wao ni yule ambaye Mtume wake alikuwa ni Muhammadﷺ, na Khalifa wake baada ya kuondoka kwake alikuwa ni Abūbakr. Na sisi (shia) hatumzingatii Mola huyo wala Nabii huyo.  Bali tunasema: Mola ambaye Khalifa wa Mtume wake baada yake ni Abūbakr si Mola wetu! Na wala Nabii huyo si Nabii wetu!."

Rejea: "Al-An'wārun-Nu'māniyyah" (Juz 2/Uk 278), chini ya mlango aliouiita "baabu fii haqiiqat diinil-imāmah".

Ndugu Msomaji! Allāh akuongoze katika haki!  kwa mara ya pili nakukukumbusha ahadi tuliyoitoa ya kuwa ni mwiko kwetu kuwasingizia na kuwabambikia wasio nayo, pamoja ya kuwa tunawachukia kwa ajili ya Allāh na kwamba haki ya Allāh kamwe hainusuriwi kwa uzushi na uongo.


Ndugu msomaji!

Hakika wamekubalina Wanazuoni wakiislamu kuwa yeyote atakayepinga nguzo moja katika zile nguzo sita za Iymani basi mtu huyo huwa kafiri.


Sasa ukiulizwa udugu wako wewe Muislamu na shia unatoka wapi utajibu kitu gani? Yeye hana haja na Mola wako, wala Kitabu chako, wala Mtume wako Muhammadﷺ!!

Kwanini wewe ujipendekeze kwake? Wataka nini kikubwa mno kutoka kwake ukiulizwa? Huna ghera wala uchungu na Itikadi yako ambayo shia anainajisi asubuhi na jioni dhahiri shahiri??


Halafu leo atokee mzandiki kama huyu Sadiq Mahd Al-Husein akurubuni akili yako kwa ibara zake za maneno yenye kuonesha uchungu alio nao juu ya umma wa kiislamu na Uislamu?  Huoni kuwa anakufanya ni sawa na mwana wa abudu au sanamu la  kuchezea watoto ambalo halina akili, macho, wala halihisi kitu?

Alafu ndugu msomaji! Nini maana ya maneno yake haya: "kwa sababu tu kundi hilo linafuata madhehebu yasiyokuwa yao na linachukua Fiqihi yao kwa Imam asiyekuwa Imam wao.."

Hapa si ilistahili Waislamu wamshukuru Mola wao kwa kusema "Alhamdulillāh"!! Kwa kuwa shetani hapa ametoa jina.

Ulishawahi kumsikia Msunniy ambaye ni Mshaafiy akisema Imam Ahmad si Imam wake? Au Mmalikiy akisema Abū Hanifa si Imam wake? Sasa kwa nini huyu ajibague mwenyewe?

Sababu ya kujibagua kwake huko ni kuwa Itikadi yake si sawa na Itikadi  ya Waislamu juu ya Maimamu.

Itikadi ya Waislamu kwa Maimamu ni kuwa wao ni watu waliosoma wakabobea, wanajitahidi katika mengi ya mambo ya kidini, yapo wanayopatia na yapo wanayokosea. Wanayopatia hulipwa mara mbili, mara kwa kujitahidi kwao kwakuwa wao ni Wanazuoni, na mara kwa kupatia kwao. Na wakikosea hulipwa mara moja  tu kwa kujitahidi kwao na kosa kusamehewa.

Na hivi ndivyo walivyowafunza watu wao.

Amesema Imam Abū Hanifah (Allāh amrahamu):

"Itakaposihi hadithi hiyo ndiyo madhehebu yangu."

Rejea: "Hāshiyat Ibn 'Ābidiin" (1/63).

Na akasema tena:

"Hakika si vinginevyo! Sisi ni binaadamu, tunasema neno leo hii, kisha tunaliacha kesho."

Kwa maana anapopata usawa  na haki lile la kimakosa (kwa kuwa wanakosea) anaachana nalo.

Amesema Imam Mālik (Allāh amrahamu):

"Hakika si vinginevyo! Mimi ni binaadamu, ninakosea na kupatia, tazameni maono yangu yatakayoafikiana na Kitabu na Sunnah yachukueni. Na yasiyoafikiana na Kitabu na Sunnah yaacheni."

Rejea: "Al-Jāmi'u" Ibn 'Abdil-Barr (2/32).

Amesema Imam Shāfi'iyy (Allāh amrahamu):

"Mtakapokuta katika vitabu vyangu kinachokwenda kinyume na Sunnah za Mtume wa Allāhﷺ, basi chukueni Sunnah za Mtume wa Allāhﷺ achaneni na niliyoyasema."

Rejea: "Al-Majmū'u" ya An-Nawawiy.Ama maimam  wa shia huwa hawakosei asilani, wamekingwa na makosa makubwa hadi  madogo.

Na wapo kwenye daraja la juu kabisa, hakuna Nabii wala Mtume anayewafikia.

Amesema Khomeni (La'natullāh 'alayhi), katika kitabu chake "Al-Hukūmatul-Islāmiyyah" Uk (52):

"Hakika miongoni mwa mambo ya lazima (kuitakidiwa) katika madhehebu yetu, ni kwamba Maimamu wetu wana daraja ambalo halifikiwi na Malaika aliyekurubishwa wala Nabii aliyepewa Utume."

Ndugu msomaji!  Hivi ni kweli kuwa watakaa pamoja wawili hawa? Mwenye Imam wake ambaye daraja lake ni hilo, na yule ambaye Imam wake anakiri kuwa yeye ni binaadamu anapatia na anakosea? Ambaye anausia kuwa kauli yake ikipingana na kauli ya Mtumeﷺ iachwe kauli yake bali ipigwe ukutani na ichukuliwe kauli ya Mtume wa Allāhﷺ!!?  Kwa maana hiyo Imam amemtukuza Mtume wake na kumpa daraja lake analostahiki. Na Imam yule wa shia yupo juu zaidi ya Mitume na Malaika akina Jibriil, Miikāiil, Israafiil na wengineo ('alayhimus-salaam).

سُبْحَانَكَ هَذا بُهْتَانٌ عَظِيْمٌ


Ndugu msomaji!

Katika yote tuliyoyaandika kwenye mfululizo wetu huu wapi kuna tuhuma za uongo kama asemavyo mwandishi huyu wa upotevu?

 Sisi tunafahamu kuwa tuhuma ni shaka na kudhania lisilo zuri. Je, katika haya tuliyoyasema dhidi ya shia wapi wamezuliwa mpaka waambiwe wale wanaowatahadharisha Waislamu wenziwao dhidi ya ushia kuwa:

"wana jazba kubwa na kuelekeza tuhuma za uongo dhidi ya kundi la Waislamu kwa sababu tu kundi hilo linafuata madhehebu yasiyokuwa yao...!!"  

Hivi, tutukaniwe Mola wetu! Nabii wetu! Khalifa wetu Abūbakr! Kisha wafanyiwe ulaghai Waislamu wenzetu tuendelee kukaa kimya!?  Kwa kukhofia kupewa sifa za jazba na kutuhumu kwa uongo!? Hilo ndo liturudishe nyuma kweli? Itakuwa Waislamu tuna akili au tuna matope? Tuna ubongo au udongo vichwani mwetu?

shia! Kwa nini msikae na kujiuliza:  "hivi kwa nini nyinyi tu!!", kwa nini wasiwe mabudha au wapagani! Mmeshindwa kujiongeza kuwa mmekuwa nyinyi kwa sababu mnafanya balaa zenu na kufru kwa ismu ya Uislamu,  na mnawaghuri na kuwadanganya Waislamu mwisho kuwatoa katika Dini yao sahihi. Lakini lau mngelibakia kwenye balaa zenu hizo kwa ismu yenu ile ya asili ya uyahudi wala msingelipatwa na haya. Tungejua tu kuwa hata  Afrika wapo mayahudi weusi.

Hivyo ni wajibu kwa wanaojua kufuru zenu na batili zenu kuwabainishia wasiojua, na hiyo ni dhima iliyopo katika shingo ya kila ajuaye, kwamba atakuwa  mas-uul mbele ya Allāh Subhānah siku ya Kiyama.


Amesema Allāh Mtukufu:

"إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِن بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ ۙ أُولَٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ" البقرة (١٥٩).

"Hakika wale wanao ficha tuliyo yateremsha -- nazo ni hoja zilizo wazi na uwongofu baada ya Sisi kuzibainisha kwa watu Kitabuni -- hao anawalaani Allāh, na wanawalaani kila wenye kulaani."

Al-Baqarah (159).

Amesema Al-Hāfidh Ibn Kathiir Al-Shāfi'iyy (Allāh amrahamu), katika kuifasiri Ayah hii:

هذا وعيد شديد لمن كتم ما جاءت به الرسل من الدلالات البينة على المقاصد الصحيحة والهدى النافع للقلوب ، من بعد ما بينه الله تعالى لعباده في كتبه ، التي أنزلها على رسله .

"Haya ni makemeo makali kwa kila mwenyekuficha yale waliyokuja nayo Mitume, miongoni mwa dalili zilizo wazi juu ya makusudio yaliyo sahihi na uwongofu wenye manufaa kwa nyoyo, baada ya Allāh Mtukufu kuwabainishia waja Wake katika Vitabu Vyake Alivyoviteremsha juu ya Mitume Wake."

Katika semi za waarabu husema:

وَباِلْمِثَالِ يَتّضِحُ الْمَقَالُ

"Na kwa kupiga mifano huwa wazi (zaidi) maneno."

Mfano:

Katika aliyoyaweka wazi Allāh ndani ya Kitabu chake Kitukufu (Qur'an), ni utakaso wa mama wa Waumini 'Aaishah (Allāh amridhie), juu ya tuhuma nzito aliyowahi kutupiwa na wanafiki zama za Mtukufu Mtume Muhammadﷺ.

Allāh Akasema:

"إِنَّ الَّذِينَ جَاءُوا بِالْإِفْكِ عُصْبَةٌ مِّنكُمْ ۚ لَا تَحْسَبُوهُ شَرًّا لَّكُم ۖ بَلْ هُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۚ لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُم مَّا اكْتَسَبَ مِنَ الْإِثْمِ ۚ وَالَّذِي تَوَلَّىٰ كِبْرَهُ مِنْهُمْ لَهُ عَذَابٌ عَظِيمٌ" النور (١١).

   " Hakika wale walioleta uwongo ni kundi miongoni mwenu.Msifikiri ni shari kwenu, bali hiyo ni kheri kwenu. Kila mtu katika wao atapata aliyo yachuma katika madhambi. Na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa miongoni mwao, atapata adhabu kali iumizayo."

An-Nuur (11).

Allah ameziita zile khabari za kusingiziwa kwa mama 'Āishah (Allāh amridhie) kuwa ni uwongo.


Na akasihi Waislamu waachane na hiyo tabia ya kinafiki akasema:

 "يَعِظُكُمُ اللَّهُ أَن تَعُودُوا لِمِثْلِهِ أَبَدًا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ" النور(١٧).

"Allāh anakuonyeni msirejee tena kufanya kama haya kabisa, ikiwa nyinyi ni Waumini!."

Na hii ni Dalili kuwa shia si waumini kwani wanamtusi 'Āishah asubuhi na jioni.

Kisha Allāh akabainisha juu ya Iymani ya 'Āishah na yule aliyetuhumiwa naye, na akakhabarisha adhabu watakayoipata wakaidi.

Akasema Allāh Mtukufu:

إِنَّ الَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ الْفَاحِشَةُ فِي الَّذِينَ آمَنُوا لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ (١٩).


"Kwa hakika wale wanao penda uenee uchafu kwa walio amini, watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na Allāh anajua na nyinyi hamjui."

An-Nuur (19).


Na akataja Subhānah kuwa kumtuhumu Mu'mini kwa ambalo yupo nalo mbali ni katika kuzifuata njia za mashetani.

 Akasema Allāh Mtukufu:

"۞ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ وَمَن يَتَّبِعْ خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ فَإِنَّهُ يَأْمُرُ بِالْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ ۚ " النور (٢١).

   "Enyi mlio amini! Msizifuate nyayo za Shet'ani. Na atakaye fuata nyayo za Shet'ani basi yeye huamrisha machafu na maovu."

An-Nuur (21).


Na akataja Allāh laana zake kwa kila atakayemrembea machafu mwanamke wa Kiislamu akiwemo 'Āishah ambaye ni Swāhibatul-Qisswah (Allāh amridhie).

 Akasema Mola Mkarimu:


"إِنَّ الَّذِينَ يَرْمُونَ الْمُحْصَنَاتِ الْغَافِلَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ لُعِنُوا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ" النور (٢٣).

"Hakika wanao wasingizia wanawake, wanao jiheshimu, walio ghafilika (na machafu), walio Waumini, wamelaaniwa duniani na Akhera, nao watapata adhabu kali iumizayo."

An-Nuur (23).

Amesema Ibn Kathiir Al-Shāfi'iyy (Allāh Allāh amrahamu):

"Hakika wamekubaliana Wanazuoni wote (Allāh awarhamu), ya kwamba atakayeendelea kumtusi ('Āishah),  na akamrembea tuhuma za machafu baada ya haya yaliyotajwa katika hii Ayah, kwamba mtu huyo atakuwa ni kafiri kwani anapingana na Qur'an."


Rejea: "Tafsiirul-Qur'ānil-'Adwhiim" katika Ayah tajwa.

Naam, anapingana na Rabbul-'Aalamiin Subhānah!!


Kisha Mola Subhānah Wata'ālaa, akabainisha kuwa 'Āishah ni mzuri,  ndio maana akapewa mzuri mwenziwe ambaye ni Mtukufu Mtume Muhammadﷺ.

Akasema Mola Mtaadhimiwa:

"الْخَبِيثَاتُ لِلْخَبِيثِينَ وَالْخَبِيثُونَ لِلْخَبِيثَاتِ ۖ وَالطَّيِّبَاتُ لِلطَّيِّبِينَ وَالطَّيِّبُونَ لِلطَّيِّبَاتِ ۚ " النور (٢٦).

"Wanawake waovu ni wa wanaume waovu, na wanaume waovu ni wa wanawake waovu. Na wanawake wema ni wa wanaume wema, na wanaume wema ni wa wanawake wema."

An-Nuur (26).


Amesema Al-Hāfidh Ibn Kathiir Al-Shāfi'iyy (Allāh amrahamu):

"Haiwi kwa Allāh kumjaalia 'Āishah kuwa ni mke wa Mtume wa Allāhﷺ ila ni pale alipokuwa mzuri, kwa sababu Mtume ni mzuri kuliko wazuri wote katika watu. Na lau angelikuwa ('Āishah) ni mbaya asingemfaa (Mtumeﷺ), si kisharia wala kimapitisho (qadar)."

Rejea: "Tafsiirul-Qur'ānil-'Ādwiim".


Amesema Ibn Al-Qayyim (Allāh amrahamu):

واتفقت الأمة على كفر قاذفها

"Umekubaliana umma juu ya ukafiri wa atakayemtupia machafu."

Rejea: "Zādul-Ma'ād" (1/106).


Na amesema Imam An-Nawawiy Al-Shāfi'iyy (Allāh amrahamu), akiwa anataja faida zipatikanazo katika hadithi ya kisa cha kuzuliwa machafu kwa mama 'Aishah (Allāh amridhie):


"Ya "arobaini na moja": Utakaso wa mama 'Āishah kutokana na kutuhumiwa kwa machafu, na ni utakaso wa kukata kabisa usoshaka, kwa ushahidi wa nassi ya Qur'an Tukufu. Lau kama kutakuwa na mtu bado amebakiwa na  mashaka juu ya utakaso huo - (Allāh Atukinge!)-Basi atakuwa ni kafiri aliyeritadi kwa makubaliano ya Waislamu wote."

Rejea: "Sharh Sahihi Muslim" (17/120-121).

Huenda mtu akajiuliza nafsini mwake: "Kwani shia wanamzungumziaje huyu mama?"

Jawabu ni kwamba shia wanamzingatia mama huyu (Allāh amridhie) kuwa ni kahaba.


 Na katika Masheikh wa shia waliomtupia tuhuma hizo nzito ni  Zaynud-Diin An-Nabātwiy mshia katika kitabu chake alichokiita:


 "Asswirātil-Mustaqem"

 katika faslu aliyoiita kitabuni humo:

"Faslu fiy Ummish-Shururi 'Āishah"

 kwa maana: Faslu inayomuhusu mama aliyejaa shari  'Āishah.


Kama alivyotuhumiwa kwa tuhuma za uzinifu na Muhsin Al-Mu'allim, katika kitabu chake:

 "An-Nawāsib" Uk 337.

Na kwamba atakuja kusimamishiwa adhabu ya uzinifu kwani alizini na Twalha.

Kama ilivyokuja katika Tafsiir yao ya Al-Qummiy chapa ya حجرية (Uk 341).

Bali wamemhukumu kuwa ni kafiri na mnafiki.

 Kama alivyosema sheikh wa shia Al-Majlisiyy katika kitabu chake:

 "Bihārul-An'waar" (22/33).


 Akasema (La'natullāhi 'alayhi):

"Ni jambo lisilofichika kwa mchambuzi mwenye weledi, yaliyomo katika hizi Ayah, katika kutaja kwake kwa uwazi kuwa 'Āishah alikuwa mnafiki pamoja  na Hafswah, bali walikuwa makafiri."

Ndugu Msomaji! Allāh akuongoze katika haki!

 Tunayaandika haya kipindi ambacho hatuna ugomvi baina yetu na shia katika mambo ya kilimwengu kwamba labda wametudhulumu vipande vya ardhi au mashamba- haasha wakalla!! - tunayaandika haya lengo letu ni kujitoa katika dhima mbele ya Allāh Siku ya Kiyama,  kwani Sharia ya Mola wetu inamtaka kila mmoja wetu baada ya kuijua haki asibaki nayo mwenyewe bali ni lazima aifikishe kwa wengine.

 Na kama kuna jambo la hatari mja ameliona na lina madhara makubwa kwa mtu mmoja mmoja au jamiii basi  ni wajibu juu yake atahadharishe Kwani adhabu kwa wafichao elimu ni kubwa mno huko umuri Kiyama. Na wale Masheikh ambao wanachanganya haki na batili, wenye kuwakumbatia mashia, bila ya kuubainishia Ummah wa Muhammad (swalla Llāhu alayhi wasallam) mabaya ya  shia, waelewe kwamba wapo katika khizyi na fedheha kwani Mola hatowaacha wallah! Na Waislamu wataendelea kuwadharau kwani wameshawajua kuwa ni watu wa maslahi wenye kuabudu dinari na dirham, Kikubwa kwao ni mkono nenda kinywani.


رحمة الله على أبي محمد عبد الله بن محمد السمرقندي القحطاني إذ يقول:

أَكْرِمْ بِعائِشَة الرِّضا مِنْ حُرَّةٍ
                بِكْرٍ مُطَهَّرَةِ الإِزَارِ حَصان
هِيَ زَوجُ خَيرِ الأَنبِيَاءِ وَبِكْرُهُ
            وَعَرُوسُهُ مِنْ جُملَةِ النِّسْوانِ
هِيَ عِرْسُهُ هِيَ أُنْسُهُ هيَ إِلْفُهُ
              هِيَ حِبُّهُ صِدْقًا بِلاَ إِدْهَانٍ

Na radhi za Allāh zimshukie Hassān bin Thābit, aliyemsifu 'Āishah akasema:


حَصَانٌ رَزانٌ ما تزن بِرِيبَةٍ
       وَتُصبحُ غَرْثى مِن لُحُوم الغَوافِل.

 

Mhusika: Al-Akh Abuu Ayman Al-Shiraaziy

Mkusanyaji: http://duaatsalaftz.net/

Nasaha

©2020 uaat Salaf Tanzania - . All Rights Reserved. Designed By Wajanjatech.Com

Search