Makala

Ukombozi Wa (Allāh) Mneemeshaji Katika Kumjibu Mshia Muovu – 09

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 
Majibu Yetu:

Allāh amrehemu Sheikh Ihsān Ilaahiy Dhahiir aliyeuawa na shia mnamo mwaka 1987, mlinganizi mpambanaji aliyejitoa nafsi yake, roho yake, maisha yake na wakati wake kwa ajili ya Allāh, katika kupambana na genge hili potevu la shia. Wajukuu wa  Ibn Sabai myahudi.

 Katika maneno yake mazuri (Sheikh Ihsaan Dhahiir) alikuwa akisema:

"shia leo hii wanajuhudi kubwa sana katika nchi za kiarabu na zisizo za kiarabu pamoja na zile nchi ambazo zina Waislamu wachache (ulaya na kwengineko), wameujaza ulimwengu kwa vipeperushi vyao na (vitabu vyao) vya uongo. Lakini (pia) kwa bahati mbaya wanaoweza kuidiriki hii kuwa ni hatari ni wachache mno. Hivyo ni wajibu kwa Muislamu anayeijua Itikadi sahihi asimame kupambana na haya mafuriko hatarishi."

Rejea: "Al-Shii'ah Shāhidiina 'Alaa Anfusihim" Uk (65).

Amesema kweli Sheikh Ihsāni Ilaahi Dhahiir (Allāh amrahamu).

Ni kweli kuwa wanajuhudi kubwa sana katika kueneza upotevu wao, kwa hali na mali na ghururi nyingi ambazo biidhnillah  tutakuja kuziainisha na kuzibaini.

Ni kweli kuwa wameingia mpaka Dola za kiarabu na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa, kama vile Iraq Syria, Lebanon, Bahrain na wameichakaza Yemen.


Ni kweli kuwa wanasambaza kwa wingi vitabu vyao, vijarida, makala na vipeperushi, kwa mustawa wa ulimwengu.

Ni kweli kuwa wanaodiriki (miongoni mwa Waislamu) hatari ya mawimbi haya ya shia ni wachache mno, wengi wao wamelala fofofo wapo usingizini wamelewa na wanakoroma kwa fadhila na ihsani za shia.

Na baadhi yao wanaonekana wakiwakingia vifua na kuwahami kuwa ni wenzetu hawa, sote tumetamka kalimah ya Laa ilaaha Illā Llāhu!! Kana kwamba neno hilo kwa aliyelitamka ni kovu isiyobanduka, au ni  kabila atakufa nalo.

Baadhi yao wanawatetea kwa hoja ya kijinga kabisa kuwa;  mbona Makkah wanaruhusiwa kuingia kama wao si Waislamu? Kana kwamba hawajui kuwa wanafiki zama za Mtume walikuwa katika jeshi lake na waliswali nyuma yake Msikitini, na hilo halikuwafanya kuwa ni Waumini bali limezidi kuwatokomeza katika moto wa Jahannam shimo la chini kabisa.

Amesema Sheikh Ihsaani Ilaahiy Dhahiir, kuwa shia wanaeneza ulimwenguni uzushi mwingi sana tena kwa bidii.


Na katika uongo wao na uzushi ni huu alioandika Sayyid wao Sadiq   Mahdi Husaini katika juhudi zake za kuusafisha ushia juu ya yale yanayoonekana kuwa kinyume na Ibada za Waislamu kama vile kusujudu kwao juu ya vidongo vinavyotoka karbala kule Iraq, akasema katika kujinasua huko:

 udongo halisi ndio ambao unafaa kusujudu juu yake kwa itifaki ya madhehebu zote za kiislamu!!

 Akiwa anaashiria kwa ufahamu wa kinyume chake kuwa haitofaa kusujudu juu ya  usiokuwa udongo.

Na akafanya talbisi zake kama kawaida yake kwa ibara ya maneno  ambayo ndani yake imeficha dhamira chafu ya kuughuri umma akasema:

 kwa sababu hiyo daima tunasujudu juu ya udongo ambao waislamu wote wanaafikiana juu ya kusihi kusujudu juu yake.

Akawaona Masunniy wote si waelewa na kwamba  mwerevu ni yeye tu   mwana wa Karbalaa!
 
Ni kweli kwamba Waislamu wameafikiana juu ya kusihi kusujudu juu ya ardhi yoyote iliyotwahara, isiyo na makaburi wala uchafu wa choo au jalala. Lakini hawakuafikiana kuwa tendo la kubeba vidongo maalumu kutoka Karbalaa na kutembea navyo ikawa mtu anapotaka kuswali anakiweka mbele yake na kusujudu juu yake. Bali Waislamu wanalizangatia hilo ni  jambo la tashiwishi kwa waswaliji Misikitini, kama ambavyo wanalizingatia kuwa ni jambo la kibid'ah. Na hukumu yao hii ni pale itakapokuwa hakuna itikadi yoyote inayoitakidiwa juu ya udongo huo wa Karbalaa. Ama kukiwa na Itikadi juu yake basi hukumu inawezakubadilika.    


Na muongo huyu Sadiq Mahdi  tutamkadhibisha hapa kwa dalili na hoja thabiti kutoka katika sharia yetu ya Kiislamu, kwamba kusujudu kupo katika hali kuu tatu:

Wanatuambiwa Wanazuoni wetu wa fiqh waliosoma wakabobea (Allāh awarehemu):

Kusujudu juu ya kitu kupo katika hali kuu tatu:

مَمْنُوعٌ، مَكْرُوهٌ، جَائِزٌ

- kusujudu kwa kuvipandanisha baadhi ya viungo vya sijda saba juu ya vingine.  

Mfano: kuuweka mkono mmoja juu ya mwingine, ukawa mmoja umegusa chini na mwengine upo juu ya uliogusa chini.

Au akaweka  mkono wake mmoja  chini kisha paji lake la uso likawa juu ya mkono huo, au kuweka mguu juu ya mwingine uliogusa chini.

Aina hii, haifai (haramu), na swala inabatilika. Kwa sababu kusujudu juu ya viungo  saba ni nguzo katika swala, na ukiupandanisha mkono juu ya mwingine au mguu juu ya mwingine utakuwa umesujudu juu ya viungo sita.

- kusujudu juu ya sehemu ya nguo  aliyoivaa mswaliji, au mkono wa kanzu yake aliyoivaa pasi na dharura yoyote kama vile baridi au vuke la joto na mfano wake.

Aina hii, ni makruhu (inachukiza tu) haibatilishi swala, pia huingia aina hii kwa wale wavaaji wa kofia wasiogusisha mapaji yao ya uso aridhini pia wavaaji wa vilemba.

- kusujudu juu ya kitu ambacho ni mubaha na hakijamvaa mswaliji, mithili ya mkeka, mswala, mbachao, shuka jani la mgomba nk.

Aina hii, ni mubaha imeruhusiwa muda wa kuwa kitu chenyewe ni mubaha na kipo katika hali ya  utwahara.

Rejea: "Naylul-Maarib Fiy Tahdhiib 'Umdatu-Twālib" pamoja na Hāshiyah yake.


Na hilo ni kwa sababu ya kuonekana Mtume ﷺ kusujudu juu ya usiokuwa udongo.

Na katika hilo imekuja hadithi ya Anas bin Mālik (Allāh amridhie), kwamba bibi yake (mzaa mama) aitwaye   Mulaykah (Allāh amridhie) alimwalika chakula Mtume wa Allāh ﷺ alichokiandaa yeye. Akaja akala (swalla Llāhu alayhi wasallam), kisha baada ya kula akawaambia:

"Nyanyukeni niwaswalishe."

Anasema Anas:

"Nikainuka kuuchukuwa mkeka wetu ambao ulipiga weusi kwa kukaliwa sana nikaumwagia maji (kuusafisha na kuulainisha), kisha akasimama (juu yake) Mtume wa Allāh ﷺ, nikapanga mimi na yatima nyuma yake, na ajuza akawa nyuma yetu."

Bukhari (380), na Muslim (658).

Hii hadithi ni dalili juu ya kufaa kusujudu juu ya usiokuwa udongo kama tulivyoona hapo.

Sasa maneno ya shia Sadiq Mahdi Husaini aliyesema:

udongo halisi ndio ambao unafaa kusujudu juu yake kwa itifaki ya madhehebu zote za kiislamu

Kama akiwa na maana kuwa kisichokuwa udongo hakifai kusujudu juu yake, basi maneno yake hayana nafasi kwa Waislamu vipenzi vya Mtume Muhammad (swalla Llāhu 'alayhi wasallam), kwani hawatoacha sunnah ya kimatendo ya Mtume wao na kufuata upuuzi wa Sadiq Mahdi.

Na hana maana nyingine zaidi ya hiyo, na lau angekuwa nayo asingelisema kwamba:

kusujudu juu ya kipande cha udongo mkavu ni dalili ya unyenyekevu na kumwogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu...

Akiwa na maana ya kuwa asiyesujudu juu ya vidongo vyao hana unyenyekevu wala hamuogopi Mwenyezi Mungu.

Sasa sijui ataweza kuthubutu kumtupia Mtume Muhammad ﷺ tuhuma nzito kama hizo au laa kwani shia hawana simile.

Hebu tutazame na hadithi hii ya  pili ambayo inamkadhibisha Sadiq Mahdi mshia:


Imepokelewa kutoka kwa Maymunah mke wa Mtume wa Allāh ﷺ Na radhi za Allāh ziwe juu yake, amesema:

"Alikuwa Mtume wa Allāh ﷺ Anaswali, na mimi nipo usawa wake, na alikuwa anaposujudu hunigusa nguo zake, na alikuwa anaswali juu ya mkeka mdogo."

Bukhari (379), na Muslim (513).

Mkeka mdogo huo ni ule uliotengenezwa kwa makuti ya mtende na mfano wake, unaitwa:  "Khumrah".

 Na sababu ya kupewa jina hilo ni kuwa mkeka huo "tukhammiru wajhal-ardh) kwa maana unaficha uso wa  ardhi pale unapotandikwa mahala ardhi hufichika,  ndio maana ukaitwa mkeka huo khumrah. Kwa maana ardhi inakuwa chini ya mkeka, na Mtume ﷺ Anasujudu juu ya hiyo Khumrah (mkeka).

Rejea: "Ma'aalimus-Sunan" ya Abū Sulaymān Al-Khattwābiy (Allāh amrahamu).

Ndugu msomaji!

Allāh akuongoe na akukinge  na balaa la shia!

Hadithi zote hizo tulizozitaja zipo kwenye sahihi Bukhari na Muslim, hazina mashaka juu ya mapokezi yake, hivyo tafakari na uchukue hatua kwani shia katika kazi zao ni kuwatia mashaka Waislamu juu ya Dini yao.

Bali tunakuta kuwa mkeka, alikuwa Mtume Muhammad ﷺ akiingia nao mpaka Msikitini kuswalia. Kinyume na alivyodai shia Sadiq Mahdi akasema:

swala zote za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) zilikuwa juu ya ardhi na alikuwa anasujudu juu ya udongo.

Waislamu tazameni talbisi na udanganyifu wa shia, kwani shia wanakuoneni kuwa nyinyi hamna maarifa wala hamuelewi mambo na kufuatilia, hivyo wanaweza kukufanyieni talbis na udanganyifu namna watakavyo.

Japo:

Ahlus-Sunnah Waljamā'ah alhamdulillah ni watu wapo makini sana, ukitaka kulijua hilo tazama vitabu vyao na juhudi zao katika kuzipembua hadithi kutoka kwa wapokezi wake, baina ya wanazozidhoofisha na kuzisahihisha kwa mujibu wa kanuni na fani ya elimu ya hadithi bali kuzipekenyua hata zile ila ndogo za kihadithi.

 Kinyume na shia wanaowaona Sunniy hawana maarifa, ambao hadithi zao hazina kichwa wala miguu, hazina hata isnadi, na wakiziwekea isnadi basi cheni za isnadi zao ni viza juu ya viza totoro.

"ظُلُمَاتٌ بَعْضُهَا فَوْقَ بَعْضٍ" النور (٤٠).

  Anapokea muongo kutoka kwa muongo mkubwa, na muongo mkubwa kutoka kwa muongo mkubwa mpaka mwisho wao.

Na amewapatia sana Imam Sha'biy 'Aamir bin Sharaahiil (Allāh amrahamu) aliyesema:

"Lau mngeumbwa katika jamii ya wanyama basi mngekuwa punda"

Na sifa hiyo ndiyo ambayo Allāh amewapa babu zao katika Qur'an, akasema:

"مَثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا ۚ بِئْسَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّهِ ۚ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ" الجمعة (٥).

Mfano wa walio bebeshwa Taurati kisha wasiibebe, ni mfano wa punda anaye beba vitabu vikubwa vikubwa. Mfano muovu mno wa watu walio kadhibisha Ishara za Allāh, na Allāh hawaongoi watu madhaalimu."

Al-Jumu'ah (05).

Na wameshabaini watu kuwa mwana wa chatu huwa  chatu.

Sasa mtoto asipofanana baba yake afanane na nani?


Ahlus-Sunnah ni watu wenye maarifa walillāhil-hamdu, ni watu wasomi  si watu punguwani kwa namna ya kwamba hawaoni au hawazingatii maneno.

Hivyo shia kusema kuwa:

Hivyo swala zote za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) zilikuwa juu ya ardhi na alikuwa anasujudu juu ya udongo Vivyo hivyo waislamu katika zama yake na zama za baada yake walikuwa wanasujudu juu ya udongo.

Hapo si kutaka kuwatia watu mchanga wa macho?

Swala za Mtume zilikuwa juu ya ardhi na alikuwa anasujudu juu ya udongo???

Shia hebu tupumzisheni kwa ihsani zenu (kama mnazo!)

Yaani mmeshindwa tu hapo kumalizia kusema kuwa alikuwa na kidongo kigumu kama kile chetu cha karbala!
 

Na mmefanya hivyo mkiwa na akili timamu kabisa mnajua mlikusudialo!

Basi kwa taarifa yenu Ahlus-Sunnah  si watu punguwani kwani wanaisoma sifa ya swala ya Mtume wao (swalla Llāhu  'alayhi wasallam), hawana haja na mafunzo yenu batili.

Alafu kusema kwamba:

Vivyo hivyo Waislamu katika zama zake na zama za baada yake walikuwa wanasujudu juu ya udongo.

Hii pia ni talbisi nyingine na udanganyifu na ulaghai.

Yaani mnataka kuwaaminisha Ahlus-Sunnah  kuwa jambo la kutumia vidongo vya Karbalaa na visivyokuwa vya Karbalaa (kama vipo) lilikuwepo zama za Maswhaba na Mataabiina!!?  Si mngetutajia kwanza ni Maswahaba gani hao?  Walioendeleza hilo jambo? Ni Abūbakr na 'Umar na 'Uthmaan mnaowalani na kuwatusi? Na kuitakidi kuwa waliritadi baada ya kufariki kwa Mtume Muhmmad (swalla Llāhu  'alayhi wasallam)? Au ni akina nani hao na riwaya zao zipo wapi?


Alafu mkisema kuwa Waislamu katika zama za Mtume na zama za baada yake walikuwa wakisujudu juu udongo mnakusudia nini? Ni udongo kama ule wenu mnaoutengeza ambao mnaubeba kwenye makoti yenu? Au walikuwa wakisujudu juu ya ardhi kubwa tu ya pale Msikitini na popote watakapokuwa safarini?


Alhaswil:

Hata ndani ya  Msikiti wa Mtume ﷺ mkeka alikuwa akiswali nao pale aupatapo.

ولو كره الكافرون

Hadithi yake ameipokea Imam At-Tirmidhiy (Allāh amrahamu), katika "sunan" yake,  ndani ya Kitabut-Twahārah, chini ya mlango:

(الحائض تتناول شيئا من المسجد).

Amesema mama 'Āishah (Allāh amridhie):

"Aliniambia Mtume wa Allāh ﷺ: "Hebu nipe mkeka kutoka Msikitini." Anasema: Nikamwambia: Mimi nipo katika hedhi. Akasema: "Hakika hedhi yako haiko mkononi mwako."

Ameipokea Imam At-Tirmidhiy (Allāh amrahamu) na akasema ni hadithi "hasan sahiih".


Kwa hadithi hizo zimetosha kuufichua uwongo wenu na ulaghai na tashkiki yenu dhidi ya Ahlus-Sunnah na sifa zote njema ni za Allāh.

 

Mhusika: Al-Akh Abuu Ayman Al-Shiraaziy

Mkusanyaji: http://duaatsalaftz.net/

Nasaha

©2021 uaat Salaf Tanzania - . All Rights Reserved. Designed By Wajanjatech.Com

Search