Makala

Ukombozi Wa (Allāh) Mneemeshaji Katika Kumjibu Mshia Muovu – 10

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 
Majibu Yetu:

Bila shaka jambo la mwenye kuswali juu ya kidongo cha Karbalaa na swala yake kupaishwa mpaka kufika  mbingu ya saba ni katika mambo ya ghaibu ambayo rai na jitihada za mtu hazina nafasi juu yake. Bali mambo kama hayo husimama juu ya wahyi wa Allāh Tabaaraka Wata'aalaa  na Sunnah za Mtume Muhammad ﷺ .

Shia! mmepata wapi habari kama hizo ambazo hazina njia  nyingine za kuzithibitisha na kuzidiriki zaidi ya Wahyi wa Allāh Subhānah??  Na kwa mujibu wa Itikadi za Waislamu ni kwamba Wahyi umeshakatika baada ya kufariki kwa Mtume wa Allāh ﷺ!!


Swali la pili:

Shia! Waislamu wanavyoamini ni kwamba viungo vya kusujudia vipo saba kwa mujibu wa hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume ﷺ aliyesema:

((أمرت أن أسجد على سبعة أعظُمٍ: على الجبهة وأشار بيده على أنفه، واليدين، والركبتين، وأطراف القدمين...)) متفق عليه.

"Nimeamrishwa nisujudu juu ya viungo saba: Paji la uso, (na akaashiria kwa mkono wake juu ya pua yake), na mikono miwili, magoti mawili, na ncha za nyayo mbili."

Ameipokea Bukhari na Muslim kutoka kwa Ibn 'Abbās (Allāh amridhie).

Sasa mbona hatukuoneni mkiweka vidongo vyenu kutoka Karbalaa katika viungo sita vilivyobakia? Ikiwa haifai kusujudu isipokuwa juu ya kidongo basi sijda ni kukamilika kwa viungo saba si uso peke yake.

Kwa Waislamu viungo vyote hivyo ni nguzo na inabatilika swala ya asiyegusisha kimoja katika hivyo ardhini.

Sasa Vipi kuhusu nyinyi? Je, mnapingana na Mtukufu Mtume Muhammad ﷺ babu yake Husein?  Na msitupe jawabu kwani jawabu lenu tunalo.

Waislamu wanajua kuwa kadhiya si suala la kusujudu juu ya udongo wala kitu gani au kitu gani,  kadhiya ni kwamba udongo huo nyinyi mnautukuza na kuuadhimisha na munayo itikadi juu yake, kuleta hoja zenu hizi feki ni kutaka tu kuuzunguka mbuyu na kuwarubuni Waislamu pamoja na  kuwafanyia talbis na udanganyifu kama ilivyo ada yenu.

Zimekuja riwaya nyingi kutoka kwenu mkizinasibisha kwa Maimamu wenu kuwa udongo huo unasujudiwa na kubusiwa, unatumika kuhesabia tasbiih, unaliwa kwa maradhi mbali mbali na kwamba ni dawa inayoliwa kwa dua:

بسم الله اللهم اجعلها شفاء من كل داء، واجعلها خيرا وبركة.

"Kwa jina la Allāh! Ewe Allāh ujaalie (udongo huu) kuwa ni ponyo ya kila maradhi, na uujaalie kuwa na kheri na baraka"

Na wote huu ni uzushi, alhamdulillah  aliyewaafu Ahlus-Sunnah  na khurāfāti zenu.

Allāh amrehemu 'Umar bin Al-Khattwab (Radhiyallāhu 'anhu!), aliyeliambia jiwe jeusi pale Ka'bah:

"Hakika mimi nafahamu kuwa wewe ni jiwe, hudhuru wala hunufaishi, na lau nisingekuwa nimemuona Mtume ﷺ Akikubusu nisingekubusu."

 Ameipokea Muslim kutoka kwa Ibn 'Umar (Allāh amridhie).

Bali mmefikia kusema kuwa udongo huu utumike kwa nia ya mlaji, kama atakula mwenye maradhi ya kaswende au mwenye corona ili apone corona lake basi utamponyesha udongo huo wa karbalaa, kama ilivyonukuliwa kutoka kwa mmoja wa mabwana wenu wa Iran aliyesadikika kusema hivi karibuni:

"Nilijihisi dalili za ugonjwa wa corona, nikachukua kiasi kidogo cha udongo wa Husein na nikapona."

Lakini haikwisha wiki moja tangu kutolewa kwa taarifa yake hiyo akafariki  bwana huyo aitwaye Hāshim Bat-Haaiy.

عامله الله بعدله.

Mmekuwa watu wa kikombe cha babu sasa!!

Mfano wao hawa katika kuangazwa kwao na Allāh na kuumbuliwa juu ya batili zao ni mfano wa Nabii wa uwongo Musaylimah aliyedai Utume zama za Nabii Muhammad ﷺ. Wafuasi wake walipotaka kuhakiki juu ya ukweli wa Utume wake walimtaka muujiza utakaosadikisha ukweli wa madai yake hayo. Akawapeleka katika kisima chenye maji machache kisha akatema mate ndani ya kisima hicho na kuwaambia watu wake mpaka kesho mtakuta kisima kimefurika kwa maji. Walipokuja siku ya pili wakakuta yale yaliyokuwepo jana pia yamekauka.
     
Na bila shaka katika hili walitaka kuwaaminisha watu kwamba udongo huo wa karbalaa unafanya kazi  mithili ya maji ya zamzam aliyoyasifia Mtume Muhammad ﷺ aliyesema:

(( ماء زمزم لما شرب له))

"Maji ya zamzam ni kwa lengo la kunywewa kwake."

Hasan. Ameipokea Ahmad katika "Musnad", na Ibn Mājah katika "Sunan".

Na akasema:

"إنها مباركة، إنها طعام طعم، وشفاء سقم".

"Hakika ni yenye baraka, ni chakula cha kukila, na ponyo ya maradhi."

Sahihi. Ameipokea Al-Bazzār katika "Musnad".

Kuhusu maji zamzam kwa mujibu wa sifa zake hakuna Muislamu mwenye mashaka na maji hayo, na Wanazuoni wetu wakubwa wamethubutu kusema kuwa maji hayo ni mujarrab.

Swali la tatu:

Ikiwa ardhi ya Karbalaa ndipo mahala alipouawa kwa dhulma Husein bin 'Aliyy (Allāh amridhie),  na alipofika sehemu hiyo aliwauliza wale alioongozana nao kuwa hapa tupo wapi? Wakamjibu: Tupo Karbulaa. Akasema hapa ni Karbun-Wabalaa (yaani: hapa ni mahali pa tabu na balaa). Kisha akafanyiwa khiyana na shia wake wakamuuwa (Allāh amridhie).

Sehemu aliyouawa kipenzi chenu kweli inafaa sehemu hiyo ienziwe na kutukuzwa??  Mkifanya hivyo mnatupa taswira kuwa nyinyi hamkuwa vipenzi vya Husein bin 'Aliyy (na ndio uhalisia), bali mlikuwa wasaliti wa Husein na wahaini wake, na nyinyi ndio mliomuuwa Husein bin 'Aliyy (Allāh amridhie).

Na hamna tofauti na waabudu misalaba, wanaouadhimisha msalaba ambao juu yake amesulubiwa Mungu wao.

Allāh amrehemu Imam Ibn  Al-Qayyim, aliyewaambia wanaouabudu msalaba:

"Enyi wenye kuabudu msalaba! Ni kwa maana ipi unaadhishwa? Au kuonekana mbaya yule atakayeutupa mbali?

 Hivi akili timamu kuna chengine ambacho itahukumu zaidi ya kuuvunja na kuuchoma msalaba huo na yule atakayeutaka?

Kama (msalaba huo) ameupanda Mola bila ya khiyari yake, na huku ikiwa mikono yake imefungwa kwa kuchomwa kwa misumari, bila shaka kipandwa hicho kinastahiki kulaaniwa. Basi kisukume mbali utakapokiona wala usikibusu.

Iweje adhalilishwe juu yake Mola wa walimwengu wote kisha wewe uuabudu (msalaba) huo?  Basi wewe ndio utakuwa adui mkubwa (wa Mola huyo)."

Na kwa kuwa lugha ya kiswahili haiwezi kikamilifu kuihudumia lugha ya kiarabu  ni vyema tukaliweka shairi la Ibn Al-Qayyim katika asili yake ili tusiichuje ladhaye na kuiharibu tamuye:

أعُبّاد الصليب لأي معنى * يُعظم أو يُقبح من رماه؟
وهل تقضي العقولُ بغير كسر؟ * وإحراق له لمن بغاه؟
إذا ركب الإلهُ عليه كرها * وقد شُدّت لتسمير يداه؟
فذاك المركبُ الملعون حقا * فدُسّه لا تبُسّه إذ تراه
يُهان عليه ربُّ الخلق طرا * وتعبده؟ فإنك مَن عداه.   

Rejea: إغاثة اللهفان


Shia! katika kuuadhimisha kwenu udongo aliouawa juu yake Imam wenu ni sawa na wakristo wanaouadhimisha msalaba aliosulubiwa juu yake Mola wao (kwa mujibu wa itikadi yao).

Alafu tujaalie kuwa inafaa kusujudu juu ya hicho kidongo kama mlivyosema kuwa:

Udongo halisi ndio ambao unafaa kusujudu juu yake kwa itifaki ya madhehebu zote za kiislamu..

Je, na kuandika jina la Husein likitanguliwa na herufi ya kunadi na kuita "Yaa Husein"  kwa maana "Ewe Husein", pia hilo lina itifaki ya madhehebu zote za kiislamu??   

Na je kumwita kwa unyenyekevu aliye mfu, ambaye hana uwezo wa kukusikia wala kukukidhia shida wala kutatua haja si jambo la kishirikina?

Amesema kweli aliyekusifuni kwa wasifu huu:

أهل البدع والزيف والمنكر
والشرك بأشكاله وبأنواعه.

 

Mhusika: Al-Akh Abuu Ayman Al-Shiraaziy

Mkusanyaji: http://duaatsalaftz.net/

Nasaha

©2021 uaat Salaf Tanzania - . All Rights Reserved. Designed By Wajanjatech.Com

Search